JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa nahodha wake Jordan Henderson licha ya kuwa ni majeruhi atapewa heshima kwa kuiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi Kuu ya England.
Liverpool, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England wanatarajiwa kukabidhiwa kombe hilo Julai 22 watakapokuwa wakimenyana na Chelsea Uwanja wa Anfield.
Liverpool imefanikiwa kutwaa taji hilo baada ya miaka 30 kumeguka bila kutwaa taji hilo na unakuwa ni ubingwa wao wa 19 hivyo wanaweka historia mpya.
Henderson yupo nje baada ya kupata majeraha ya goti kwenye mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Brighton.
"Tutafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba tunakuwa na mchezaji Henderson, tutahakisha anakuwa na nafasi ya kupata heshima yake kwa kubeba kombe hilo," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment