MOTO wa kikosi cha Arsenal umekuwa hauzuiliki kwa sasa kwenye mechi kubwa na ngumu baada ya kuanza kwa kuwanyoosha kwa tabu mabingwa Liverpool mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Usiku wa kuamkia leo wamewanyoosha mabingwa wa Kombe la FA, Manchester United mabao 2-0 Uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.
Mabao ya ushindi yalifungwa na nahodha wa Arsenal, Pierre Emerick Aubemeyang ambaye alianza kucheka na nyavu dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza na bao la pili alipachika kipindi cha pili dakika ya 71.
Tayari safari ya bingwa mtetezi imeisha ndani ya Kombe la FA hivyo fainali Arsenal anamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Chelsea na Manchester United unaotarajiwa kuchezwa leo usiku ili ajue atacheza na nani kati ya vigogo hao wawili.
Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal aliweza kukiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi huo mbele ya kikosi cha bosi wake wa zamani, Pep Guardiola ambaye alifanya naye kazi ndani ya City.
0 COMMENTS:
Post a Comment