July 13, 2020






NA SALEH ALLY
USIJALI nani alionekana bora au kushinda au kupoteza baada ya mechi ya jana ya watani Simba na Yanga.

Unajua namna kulivyokuwa na tambo kabla ya mechi hiyo ya jana ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports kati ya watani hao na kila upande ulikuwa unajiamini.

Baada ya Yanga kufanya vizuri zaidi katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na kubeba pointi nne kati ya sita huku Simba wakibeba moja tu, walionekana kujiamini kupita kiasi na walikuwa na haki ya kufanya hivyo kwa kuwa rekodi ya hivi karibuni inaonyesha wao ni bora zaidi ya watani wao.

Watani wao walikuwa wanaamini kwa takwimu, kweli ni sahihi kwamba wao wana kikosi bora zaidi ya Yanga. Lakini walishindwa kulidhibitisha katika mechi hizo ambazo ya kwanza iliisha kwa sare ya mabao 2-2 baada ya Yanga kusawazisha mara mbili na ya pili, Simba wakalala kwa bao 1-0 na Yanga wakatandaza soka safi la kitabuni. 

Hakuna ubishi tena kwamba kila baada ya mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba, maisha huwa yanaendelea kama kawaida. Maisha huwa yanakuwa na nafasi nyingine ya kujaribu mambo mengine na kunakuwa na nafasi nyingine ya Yanga na Simba kukutana.

Mfano mzuri, Simba na Yanga wamekutana mara tatu katika msimu mmoja. Mechi mbili za ligi kuu na moja ya Kombe la Shirikisho, kama burudani ya Kariakoo Dabi imekuwa ni ya kutosha kwa msimu huu na ndani ya mwaka mmoja tu wamekutana mara tatu na kuna nafasi ya kukutana mara nyingine, huenda katika ligi miezi ya mwisho ya mwaka huu.
Nasisitiza sana suala la kwamba kuna maisha baada ya Simba na Yanga kwa kuwa kila baada ya mechi hii, wako wanapoteza kazi zao, wako wanajengewa chuki, wako wanaonekana ni wasaliti wako wanahisiwa kadha wa kadha na wako wanaolalamikiwa au kulaumiwa kupindukia.

Mchezo kama huu, kwa kuwa macho na masikio ya wengi yanaelekezwa kuna haja ya kujifunza na kukubali kuwa mechi hiyo ni kama nyingine za Ligi Kuu Bara lakini hii inakuwa gumzo kutokana na historia. Lakini haizuii kuwa mechi ya soka na ambayo baada ya hiyo nyingine zinafuatia au maisha yanaendelea.

Utaona hakuna timu ambayo hukubali kufungwa bila ya kumtafuta mchawi. Anaweza kuwa mchezaji, anaweza kuwa kiongozi au mwamuzi, anaweza kuwa yeyote yaani ilimradi watu hutengeneza kituo cha kushushia hasira zao baada ya kupoteza mchezo au kushindwa kushinda.

Kama unakwenda katika mechi, kitakachotokea lazima kiendane na sare, kushinda au kufungwa na bahati nzuri kila anayekwenda uwanjani au kufuatilia mchezo anajua kabisa kati ya hayo matatu yatatokea na sababu za kutokea tunajua sote, lazima iwe kosa au makosa ya mchezaji au wachezaji.

Bila makosa, hakuna timu ingekuwa inashinda dhidi ya mwenzake na kama ni makosa lazima wawe wale wanaocheza mule ndani, kuanzia wachezaji hadi waamuzi. Hata uzuie vipi, ili moja ifunge lazima kuwe na kosa au makosa.

Sasa malumbano yanayopelekea wengine kuwachukia wengine, wengine kufukuzwa kazi au kuonekana kama ni maadui, ni mambo yaliyopitwa na wakati na yanayoonyesha namna ushabiki ulivyotumeza badala ya furaha yenyewe ya mpira na kuamini suala la maisha kuendelea baada ya mechi kama hiyo ya jana.

Simba na Yanga ni mchezo, hauwezi kuwa zaidi ya maisha ya kila siku. Mechi ikipita, acha liwe gumzo na burudani lakini chuki za kipuuzi, watu kuamini kashfa na matumizi ndio hoja, ni kupungukiwa uwezo wa kufikiri kwa usahihi. Tuanzie leo kubadilika na kuamini, mechi imepita jana, leo ni maisha mapya.

15 COMMENTS:

  1. nyie waandishi mnachangia kuivuruga Yanga, mnatumika na upande wa pili kuihujumu Yanga, hasa kipindi cha usajili na mnavuruga saikolojia ya wachezaji wa Yanga. Hongera mwandishi naona una furaha baada ya Yanga kufungwa, kachukue chako Simba kwani umechangia pia ushindi wa jana.

    ReplyDelete
  2. Salehe Ally kafunga goli ngapi jana?Wacha kutafuta mchawi. Mechi ya jana tulizidiwa sana na tushukuru kwamba magoli yangeweza kuwa zaidi ya manne. Simva walituzidi kika idara. Kipindi cga kwanza hatukuwa na shots in target hata moja.Tukubali ukweli kwamba Simba wana timu nzuri kuliko sisi.

    ReplyDelete
  3. Najua Saleh, Morandy na waandishi wengine wa gazeti hili ni YANGA. Lakini wanachokieleza ni cha msingi. Maisha lazima yaendelee. Chuki tusizipe nafasi. Wachezaji wa Yanga walijituma na kucheza vizuri isipokuwa Simba ilikuwa bora zaidi. Tujenge kukubali ukweli huo na tusonge mbele.

    ReplyDelete
  4. Ilipofungwa simba goli moja wewe mwandishi ndio ulikuwa mstari wa mbele kila siku muuaji wa simba na stori za morisson kila siku. Leo imekuwaje unatihamasisha maisha bado yapo? Acha na wap wapewe vidonge vyao walizidi kelele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu salehe ni Yanga, Kweli Simba tulipofungwa, alifurahi sana kaongelea mwezi kibao, hata siku moja kabla ya Mechi, kila saa Morison, Morison, Leo hii hata kuandika hawezi, atuachee tuwa cheke mwaka mzima

      Delete
    2. Salehe ally si yanga ni Simba lia lia ila tu sisi washabiki tuna miemko yetu alishawahi kuulizwa na kituo kimoja cha habari (EFM - SPORTS HQ )akasema yeye ni Simba kwa hiyo kusema yeye Yanga ilo tutakuwa tunamuonea mimi mwenyewe simba damu

      Delete
  5. Akishinda Yanga kila siku habari ni hizo hizo, sasa leo lipi limetokea mambo yawe kawaida?, Waache waseme kama ulivyokuwa unaandika na kusema!.

    ReplyDelete
  6. Usitetee ujinga. Kila siku ulikuwa unakuja na stori za muuaji wa Simba. Jana Utopolo kapigwa 4G ohh maisha yaendelee.Maiaha yanaendelea siku zote. Au 4G imekukera hutaki itajwe?

    ReplyDelete
  7. Nasikia bila kutoa hela hawajamaa hawashindi.

    ReplyDelete
  8. Ubingwa was kutengenezwa Kamara corona

    ReplyDelete
  9. acha uboya wewe mwandishi story za muuaji wa simba, mkuki wa sumu na kadharika zimeishia wapi bwege wee acha unazi wa kipuuuzi zingatia weledi na usawa

    ReplyDelete
  10. Kiukweli hata aina ya kukumbatia wachezaji imeonekana kwa Yanga. Niyonzima na Morrison sijui kwa nini walipangwa. Unaona vijana wetu Kaseke na Feisal Toto walivyopigana ila hawakuwa na support yoyote ile. Ukiangalia hata Shishimbi bora alivyoingia Yondani na kusaidia beki line kuelewana kidogo licha ya bao tatu kuingia, ila alipunguza maana niliona kama nane hivi.

    Kiukweli kisaikolojia Yanga haikuwa kwenye mood ya mchezo na ndo mwanya wa Simba ukapia hapo. Maisha yapo baada ya Simba Vs Yanga ila mechi ya timu kubwa kama hizo kufungwa bao hizo 4, wacha watu waendelee kuongea. Maana kabla ya hapo majembe manne yameandaliwa kuiua Simba sasa sijui yalikuwa butu?

    ReplyDelete
  11. Salehe kaa mbali na furaha ya Wanasimba, kama 4G imekuuma, tulia

    ReplyDelete
  12. Majembe manne yamegeuka 4 G.Championi wacheni unazi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic