MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/20.
Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC alioingia nao fainali.
Bocco amefunga jumla ya mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara na timu yake ikitwaa ubingwa wa tatu mfululizo.
Imetwaa ubingwa ikiwa na mechi mkononi ambapo zoezi zima la kupewa taji la ubingwa lilifanyika Lindi baada ya kumaliza mchezo wa ligi dhidi ya Namungo.
Mchezo huo uliochezwa Jalai 8 timu zote zilitoshana nguvu ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment