July 26, 2020



LEO Julai 26 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kufika tamati huku mtifuano mkubwa ukiwa ni kwenye timu ambazo zinapambani nafasi ya kubaki ndani ya ligi pamoja na kucheza playoff.

Ishu ya ubingwa tayari imeshafungwa kwani Simba ni mabingwa kwa msimu wa 2019/20.

Cheki namna ratiba ilivyo na hesabu zitakazochezwa leo ndani ya dakika 90:-

Alliance FC ipo Nafasi ya 18 na pointi 42, imepoteza mechi 15 na imeshinda 10 ikiwa na  sare 12 haina uhakika wa kubaki nakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 4 ina uhakika wa kubaki ikiwa imeshinda 17, sare 13,poteza 7, pointi 64 pale Uwanja wa Nyamagana Mwanza.
 
 Mbao FC haina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 17, shinda 11, sare 9, poteza 17, pointi 42 inakutana na  Ndanda FC ambayo nayo haina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 19, shinda 9,sare 14,poteza 14, pointi 41 pale Uwanja wa CCM Kirumba , Mwanza.

KMC FC ina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 12, shinda 13, sare 7,poteza 17, pointi 46 inakutana na Mbeya City ambayo haina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 16, imeshinda 11, sare 9,poteza 17. Pointi 42, Uwanja wa Azam Complex -Dar es Salaam.

 Singida United ina uhakika wa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ipo nafasi ya 20, shinda 4, sare 6, Poteza 27. Pointi 18 inakutana na Biashara United ina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 10, shinda 11, sare 14, poteza 12. Pointi 47, Uwanja wa Liti -Singida.

 Mwadui FC haina uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 14, pointi 44   inakutana na Kagera Sugar yenye uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 8, pointi 52 Uwanja wa  Mwadui Complex -Shinyanga.

 Polisi Tanzania ipo nafasi ya 5 ina pointi 55 ina uhakika wa kubaki inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 85 Uwanja wa Ushirika -Moshi.

 Coastal Union ipo nafasi ya 6 pointi 53 dhidi ya  JKT Tanzania iliyo nafasi ya 8. Pointi 51 pale Uwanja wa Mkwakwani -Tanga, zote zinauhakika wa kubaki.

 Mtibwa Sugar, nafasi 15, pointi 42 haina uhakika wa kubaki dhidi ya Ruvu Shooting yenye uhakika wa kubaki ikiwa nafasi ya 11 pointi 47, Gairo -Morogoro.

 Tanzania Prisons ipo nafasi ya 9,pointi 48 dhidi ya Azam FC iliyo nafasi ya pili. Pointi 69, Uwanja wa Sokoine -Mbeya

Lipuli FC haina uhakika wa kubaki ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 44 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya 3. Pointi 69
 Uwanja wa Samora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic