JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho kipo nyuma ya mafanikio ya kikosi hicho ni ushirikiano pamoja na sapoti ya mashabiki.
Simba imetwaa ubingwa mara tatu mfululizo na kufanya taji hilo liwe lao kabatini jumlajumla kwa mujibu wa kanuni.
Ilianza msimu wa 2017/18,2018/19 na 2019/20 wakiwapoteza wapinzani wao wakubwa ambao ni Yanga na Azam FC.
"Tunafuraha kutokana na kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea katika kutwaa ubingwa jambo ambalo kwetu ni furaha pamoja na mashabiki kiujumla.
"Kikubwa kinachotufanya tufikie mafanikio yetu ni kujituma pamoja na nguvu ya mashabiki, sapoti kubwa ambayo tunapewa imekuwa ikitufanya tuzidi kupambana, tumefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara bado tuna kazi ya Ligi ya Kombe la Shirikisho, " amesema.
Simba itamenyana na Namungo FC, Uwanja wa Nelson Mandela Agosti 2.

0 COMMENTS:
Post a Comment