UONGOZI wa Simba umesema kuwa unaamini aina ya wachezaji walionao hivyo wanaamini watapata matokeo chanya mbele ya Yanga kwenye mchezo wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku ikiwa ni dabi ya tatu kwa msimu huu wa 2019/20 kuwakutanisha watani hao wa jadi.
Januari 4, Simba ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Machi 8 Yanga ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na Bernard Morrison hii inakuwa ni kwenye ligi kisha dabi ya tatu inatarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ya Mungu ni mengi hasa kwenye mpira ila kwa namna walivyojipanga wanaamini watapata ushindi.
"Kweli ni mchezo mgumu kwetu dhidi ya Yanga kwani wao wanahitaji zaidi ushindi kuliko sisi, ukitazama tuna nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa tofauti na ilivyo kwao hivyo watakuja vizuri.
"Sisi tuna amini kwamba kiubora na namna wachezaji wetu walivyojiandaa basi ushindi utakuwa upande wetu lakini mambo ya Mungu ni mengi naye ana maajabu yake.
"Mashabiki wasisahau kwamba kuna utaratibu wa kufuata hasa kuzingatia kanuni za afya kujikinga na Corona na tayari inatakiwa kuwe na nusu ya mashabiki hilo lipo wazi muhimu kuwahi kupata tiketi mapema kisha kujitokeza uwanjani," amesema.
Msimu huu Simba haijapata ushindi mbele ya Yanga kwa uwa iliambulia maumivu ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa hivyo ina kazi ya kufuta makosa kesho taifa jambo litakaloongeza ugumu wa mechi.
Miongoni mwa viungo wazawa ambao wamekuwa kwenye ubora wao ndani ya Simba ni pamoja na Hassan Dilunga mwenye mabao saba na pasi tatu za mabao huku Shiza Kichuya naye taratibu akianza kuingia kwenye mfumo kwani amefunga bao moja ndani ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment