LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anazitambua mbinu za wapinzani wake Simba hivyo hawatamsumbua kesho Taifa.
Simba itakutana na Yanga kesho, Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unaoatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Eymael amesema.“Ukicheza na mpinzani wako kama Simba lazima umheshimu, lakini uwe makini katika kuziba nafasi zako ili wao wasipasiane kwenye lango lako.
"Simba wanashauku ya kutufunga, kwa hiyo watajisahau na sisi tutatumia kujisahau kwao kuwafunga. Mashabiki waje kwa wingi, maana naahidi kucheza soka lenye burudani,”.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Kaitaba jambo linalompa hali ya kujiamini Eymael.
Simba wao ambao ni mabingwa wa ligi wanaingia uwanjani wakiwa wametoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Namungo FC, Uwanja wa Majaliwa,Lindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment