July 12, 2020


USHINDI wa mabao 4-1 ambao wamepata Simba leo, Julai 12 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali wa Kombe la Shirikisho unawapa nafasi ya kukutana na Namungo FC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Sumbawanga. 

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imepata ushindi huo kupitia kwa Gerson Fraga dakika 21, Clatous Chama dakika ya 50, Luis Miqussone dakika ya 52 na Mzamiru Yassin dakika 88.


Yanga ilipata bao la kufuta machozi dakika ya 70 kupitia kwa Feisal Salum aliyepiga shuti lililomshinda Aishi Manula mlinda mlango namba moja wa Simba.


Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars. 


Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga ulikuwa na ushindani mkubwa na bao lilipatikana kipindi cha pili kupitia kwa Edward Manyanya.


Luis Miqussone,  kiungo wa Simba amesema kuwa ushindi walioupata ni zawadi kwa mashabiki pamoja na uongozi kiujumla.

13 COMMENTS:

  1. Na Zahera nae eti Yanga itashinda. Ama Mnyama kwa kweli katufurahisha. Kile ni kipigo cha mbwa mwizi kwa haki ya bingwa wa kihistoria timu ya wananchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Muuaji wa simba vp maana ndio ilikuwa habari yenu sijui mtakuwa mnaandika nn

      Delete
  2. Nadhani wakubali tuu kuwa timu yao ni dhaifu mno uwanjani, wamekuwa wakieneza uongo uongo ili mashabiki watulie sasa sijui itakuwaje. Kama simba inabebwa basi mbebaji ni yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii ni dhahiri SIMBA ina kikosi kipana na bora.Wamedhirisha kuwa mpira ni uwanjani tena mbele ya waamuzi sita.Next time tunaomba waamuzi watoke nje ya nchi kama hatukushuhudia kila mchezaji wa Yanga atarudi kwa boda boda makwao.Hiyo ndio mwana ya kulitaka mwana kulipata.Aaah wacha tupumue.

      Delete
  3. Rodrick hadithi ya muuaji wa Simba sasa finito. Habari ya mujini ni 4G.

    ReplyDelete
  4. tusisahai matokeo ya Jumla!Katika masaa 48 yaliyopita Simba 9 vs Yanga 2
    Simba Queens 5 vs Yanga Princess 1, halafu Simba 4 vs Yanga 1

    poleni sana Yanga

    ReplyDelete
  5. Zahera alisema Simba itafungwa sasa kapata bakora tamu sana.

    ReplyDelete
  6. Haooooo GONGOWAZI kazi yao kusifiwa kwenye magazeti na huyo mpumbavu wao nugaz na kesho muwasifie tena 4G imewatosha tena zilikuwa 7 bahati yenu leo tulipanga watoto ndio wawafunge kandambili nyinyi huyo morson wenu vipi leo? GONGOWAZI aka vyura

    ReplyDelete
  7. Sijaridhika zilitakiwa 7.4G inatosha kwa sasa.

    ReplyDelete
  8. wanasimba wenzangu hivi hili soka wanalocheza Simba ni kazi ya Sven Van au la kocha Uchebe?

    ReplyDelete
  9. Sasa Yanga ikae kitako wakitafute kipi kinachowaumiza. Kocha mzuri na wachezaji nyota wa tuwi la Kwanza wanao, mishahara ya miezi miwili wamelamba na huku wakiahidiwa kumi na nane milioni na Mnyama kumi na tano tu kama walivo tangaza wao wenyewe. Hela hii yote inavuja kama maji ndani ya debe bovu. Wanaotowa hela wanaotaka kuona faida yake na tunachokiona kwa mashabiki ni zomeazomea na kusherehekea lile bao la Morisson ambae Jana baada ya kuondolewa kaingia mitini na haijulikani kaelekea wapi na vituko gani atavianza, lakini atalaumiwa Mnyama kwa kumrubuni na kucheza chini ya kiwango, lakini sio yeye tu, timu nzima ilikuwa ovyo lakini tutaona.

    ReplyDelete
  10. Na yule Haruna Niyomiza aliejiumiza nae eti aliimba apewe nafasi ya angalau dakika 45 eti amuue Mnyama na ndie hakuonekana kabisa

    ReplyDelete
  11. Utopolo lazima wajue Simba ni next level.Hakuna timu ya Tanzania ta kushindana na Simba. Mtapunguza magoli tu.Jana zilirskiwa ziwe 7.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic