Tunduru Korosho ya Ruvuma leo wameibuka mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2020 mbele ya Kurugenzi FC ya Simiyu.
Timu hiyo Imeshinda bao 1-0 mbele ya Kurugenzi FC kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma.
Bao pekee la ushindi leo lilifungwa na Hamza Malanda dakika ya 103 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Ushindani ulikuwa mkubwa na ndani ya dakika 90 za awali ngoma ilikuwa bilabila.
0 COMMENTS:
Post a Comment