UONGOZI wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 Simba umesema kuwa ,kiungo wao Luis Miquissone amezivutia timu nyingi nje ya nchi ambao wamekuwa wakiuliza kuhusu huduma ya nyota huyo.
Luis ambaye amebatizwa jina la Mmakonde amefunga jumla ya mabao matano kwenye ardhi ya Bongo katika mashindano yote ikiwa ni ndani ya ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.
Ametupia mabao manne ndani ya ligi na pasi moja huku akiwa amefunga bao moja kwenye Kombe la Shirikisho, Julai 12 mbele ya Yanga.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amekuwa akiuliziwa na marafiki zake kutoka Ulaya ambao ni mawakala kuhusu kumpata nyota huyo.
"Rafiki zangu watatu ambao ni mawakala wakubwa Ulaya wameshaniulizia kuhusu huyu Mmakonde, na tajiri nishamwambia, but (lakini) Simba inahitaji Quality players (wachezaji bora) kama hawa ili kufanya vema katika Champions league msimu ujao.(Ligi ya Mabingwa Afrika).







Anachokifanya Louis sio kigeni ila vijana wetu ni wavivu hasa kiakili katika kukuza viwango vyao Mfikirie Kuchuya anatofauti gani na Louis? Na yuko wapi sasa kichuya? Starehe,kuvimba kichwa mapema na kusikiliza fitna za kijinga. Siku zote tunasema hawa wachezaji wa wageni wanaichukulia simba kama fursa ila vijana wetu wao wanachukulia powa sasa mawakala kwanini wasiulizie vijana wetu wazawa kutoka ligi yetu nzima?
ReplyDeleteInamaana hakuna mzawa mwenye kiwango cha Louis na hii sio majungu bali wao wazungu ndio wameona huko waliko na ndio ukweli na wala isiwe chanzo cha louis kufanyiwa hasada na fitna katika maisha yake ya soka hapa Tanzania bali vijana wetu wanatakiwa kujifunza kutoka kwake. Jambo moja la kujifunza kutoka kwa Louis kwa vijana wetu ni kule kujiamini kwake uwanjani na kuheshimu mpira kuwa ndio maisha yake.
Manara amegeuka dalali wazungu gani wasiojua taratibu badala ya kufata uongozi wanamfata msemaji wa timu
ReplyDeletePovuu tayarii...🏃🏃🏃🤸
ReplyDeleteManara ni sehemu ya uongozi wa Simba
ReplyDeleteYuko makin
ReplyDelete