July 27, 2020


UONGOZI  wa Yanga umesema kuwa suala la mchezaji wao Bernard Morrison kutokuwa na timu kwa sasa kambini, Iringa huku akionekana akicheza mechi za mchangani maarufu kama ‘ndodo’ linashughulikiwa.
Morrison raia wa Ghana amekuwa kwenye mvutano mkubwa na Klabu ya Yanga kuhusu suala la mkataba wake ambapo yeye anadai kwamba mkataba wake ni wa miezi sita na umemalizika huku Yanga ikieleza kuwa ana dili la miaka miwili.
Julai 12 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Morrison mwenye mabao matano na pasi tatu za mabao kuonekana na Yanga ilikuwa ni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba wakati Yanga inapoteza kwa kufungwa mabao 4-1.
Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa nyota huyo hajaripoti kambini huku suala lake likifuatiliwa kwa ukaribu.
“Morrison ni mchezaji wa Yanga hilo lipo wazi kwa kuwa kwa sasa inaonakena anaonekana akicheza mtaani suala hilo linafuatiliwa kwa ukaribu kwani kuna sheria za kazi hivyo namna ambavyo zitaeleza hatua juu yake itachukuliwa,” alisema Mwakalebela.
  

4 COMMENTS:

  1. Hili suala yanga limewazidi nguvu, bora tuu waliache ukweli usemwe. Vipi suala kocha kuporomosha matusi?

    ReplyDelete
  2. Hakuna wanachoweza kumfanya Morrison. Ameipanda klabu yetu kichwani. Mtu huwa anavuna anachokipanda.

    ReplyDelete
  3. Kwakifupi Morrison anafanya utovu wa Nidhamu ili avunje mkataba, Viongozi sio watoto wadogo, kumbukeni ukivunja mkataba kunastahiki zake anatakiwa kulipwa, pia itakua advantage kwa wapinzaniwa Yanga kumchukua kirahisi, tusubiri dirisha la usajili liishe ndio tutaona malengo halisi ya viongozi.

    ReplyDelete
  4. Team Kama Simba unasubiria kwa karibu wakimuacha imchukue, lkn wakumbuke mtu asiekuwa muungwa siku zote hakosi hila, huenda wadilione Hilo kwasasa lkn muda utaongea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic