July 23, 2020


LUC Eymael,raia wa Ubelgiji, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hataki kusikia kabisa jina la kiungo wa Yanga, Bernard Morrison.

Maamuzi hayo magumu yametokana na Eymael kutofurahishwa na matendo ya nyota huyo ambaye inaelezwa kuwa anawindwa na watani zao Simba.

Morrison amekuwa kwenye mvutano na viongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba, yeye anadai mkataba wake ulikuwa ni wa miezi sita na umemeguka huku Yanga wakieleza kuwa ni kandarasi ya miaka miwili.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa ikiwa Morrison hana mkataba na Yanga basi anapewa ruhusa ya kusaini anakohitaji.

"Kama yeye ni mchezaji huru basi aende kusaini anakohitaji maana tumechoka sasa kuzungumzia suala lake, aende tena nasema aende akasaini haraka," alisema.

Eymael amesema kuwa kwa sasa hataki kuskia jina la mchezaji huyo na hataweza kuzungumzia masuala yake.

"Kuhusu Morrison kwa sasa siwezi kuzungumzia masuala yake na wala sitaki kuskia jina lake atamalizana na uongozi," amesema.

Bado Morrison hajajiunga na Yanga kwa sasa tangu atolewe Uwanja wa Taifa dakika ya 64 ambapo alisepa uwanjani na bodaboda.

3 COMMENTS:

  1. Huyu jamaa Morissoni ni chizi sana kumbe alisepa na bodaboda sio mchezaji labda anavuta bangi

    ReplyDelete
  2. tatizo viongoz wakiwepo wakina nugaz bumbuli wasemaji wao walimwabudu sna kwa hyo acha waone madhara yake

    ReplyDelete
  3. Sio kumuambudu unavyofanya vzr unapewa credit zako ila usivimbe kichwa wala kuharibu ndio haya yanatokea hata watia Nia yaani attitude za most africans ni the same na hii yote ni njaa Yaani mtu unayumbishwa unashindwa kusimamia issue zako unafikiri watu waliokuwa successfully kwenye chochote hata soccer walifanya ujinga huu wachezaji wa hii ligi wengi hawana discipline utaona tu wanavyomzonga refa wakati wa games Yaani bado amature mno

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic