July 18, 2020

YANGA leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Julai 18.

Yanga ilianza kuandika bao la Kwanza dakika ya 27 kupitia kwa Feisal Salum ambalo lilidumu mpaka muda wa mapumziko.

Dakika 45 za kipindi cha Kwanza zilikamilika kwa Yanga kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa mbele kwa bao hilo la Fei Toto.

Kipindi cha pili Mwadui FC ilisawazisha kupitia kwa Yahya Mbegu dakika ya 56 na kufanya ubao usomeke 1-1.

Mwadui imeshindwa kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wao uliopita wa Ligi na kuishia kuambulia pointi moja.

Yanga inafikisha pointi 68 huku Mwadui wakifikisha pointi 41 ndani ya Ligi wote wakiwa wamecheza mechi 36.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic