July 19, 2020


KOCHA Mkuu wa As Vita, Frolent Ibenge ambaye inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za Simba inatajwa kuwa kocha huyo ataambatana na kiungo wa timu yake, Jeremy Mumbere ambaye amesema kuwa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kujiunga na Simba.

Mumbere amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Kocha Ibenge ndani ya AS Vita ambao wanaweza kukutana na Simba itakayoshiriki katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika ‘CAF’ kwa msimu ujao.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema kuwa timu hiyo itafanya usajili wa wachezaji wa maana ili kuhahikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michuano ya kimataifa tofauti na msimu uliopita ilipofanya vibaya.

Akizungumzia juu ya suala hilo,Mumbere alithibitisha kuwa katika mazungumzo na Simba huku akiweka wazi kuwa muda si mrefu watamalizana kwa kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili.

“Nipo kwenye mazungumzo ya muda mrefu na Simba,tumefikia sehemu nzuri,lakini bado hatujamalizana,natarajia kuona usajili wangu ukikamilika siku za hivi karibuni baada ya ligi ya Tanzania kumalizika.

“Kuhusu kocha wangu Ibenge kutakiwa na Simba nimesikia tetesi tu zikisema hivyo lakini bado hakuna taarifa kamili kuhusu yeye kujiunga na Simba ninachokifahamu kuhusu yeye bado mwalimu wa AS Vita,”alisema Mumbere.

1 COMMENTS:

  1. Hapo mmesem la akili lakini Mnyama Bana Katika mambo yake kimyakimya haropoki utastukia keshafanya huku wengine wakilia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic