July 12, 2020

WILFRIED Zaha nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Crystal Palace amesema kuwa amepokea jumbe mbili ambazo zilikuwa zinaeleza kuhusu ubaguzi wa rangi wakati wa kuifuata Aston Villa mchezo wa Ligi Kuu England. 

Leo Julai 12, Aston Villa anakokipiga Mbwana Samatta ipo kazini kumenyana na Crystal Palace. 

Mshambuliaji huyo amesema kuwa alipokea meseji mbili ambazo zilikuwa zinambagua kutokana na rangi yake jambo lililompotezea furaha.

"Nilipokea meseji mbili ambazo zote zilikuwa zinasema kwamba sitafunga mbele ya Aston Villa kwa kuwa rangi ni nyeusi jambo ambalo sijalipenda na ni mbaya kwangu na dunia,".

Uongozi wa Premier league umesema kuwa kwa sasa unafanyia uchunguzi suala hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic