IMEELEZWA kuwa Manchester United ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya beki wa Klabu ya RB Leipzig, Dayot Upamecano kwa ajili ya kuongeza nguvu msimu ujao wa 2020/21.
Kocha Mkuu wa United, Ole Gunnar Solskjaer yupo kwenye mpango wa kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa kwenye tatizo la umakini kwa msimu wa 2019/20
Lengo la kocha wa United ni kumuongezea nguvu nahodha wa kikosi hicho, Harry Maguire ambaye ndiye tegemeo kwa upande wa ulinzi ndani ya kikosi hicho.
Kwa mujibu wa ESPN, Solskjaer anaamini kwamba atakamilisha dili hilo mapema kabla ya Oktoba 5.
Tayari nyota huyo mwenye miaka 21 anayeshiriki Ligi ya Bundesliga amesaini mkataba mpya na timu yake ambayo ilitiga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutolewa na PSG ya Ujerumani hivyo italazimika kutoa pauni milioni 53 kwa ajli ya ada ya kumpata nyota huyo .
0 COMMENTS:
Post a Comment