August 31, 2020

 


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amewaomba mashabiki na watanzania wampe heshima kabla hajatangulia mbele za haki kwa kuwa amefanya mengi makubwa kwa sasa katika kuutangaza mpira.

Haji ameandika namna hii:-Watanzania nipeni heshima yangu walau kidogo, ntaumia sana nikifa mkaja kusoma salaam zenu makaburini kunielezea wasifu na sifa zangu,huku mkinipamba kwa tenzi na shairi nzuri nzuri.

"Leo Yanga wametumia washehereshaji watano katika jambo ambalo nalifanya peke yangu always!

"Mimi napenda heshima tu ,,msinisifu ila mtambue nimewachangamshia mpira wenu, waliokuwa baridi nimewafanya walau nao wachangamke,japo bado wanafanya uchale tu mbele ya Simba.

"Wanasimba wenzangu tujishukuru kwa tulipo na wenzetu walipo,,.hawana chembe ya 'Creativity',(ubunifu),hawajui hata 'wat they want'(nini wanataka).

"Hebu nyie na Watanzania wote nipeni japo heshima yangu na management ya Simba pamoja na Bodi ya Klabu chini ya tajiri wa mpira bwana MO kwa haya tuliyoyafanya kwa mpira huu ndani ya nchi hii!

"Leo Afrika nzima inazungumzia Simba Day,labda Kesho itazungumza kuhusu anguko la Commandoo wa kimakonde 'but behind it' (nyuma yake) kuna kazi kubwa imefanyika.

"Na hiyo kazi imefanyika kutokea Simbaa.Narudia mimi napenda sifa ila nazitaka sasa, sifa niikiwa kaburini au katika jeneza kwangu ni naniliu tu.

"Akili zangu za usiku nazijua mwenyewe."

17 COMMENTS:

  1. Manara Bhana!!!! Vituko kila kukicha

    ReplyDelete
  2. Brother Manara uko fit sana na umekuwa creative sana katika maendeleo ya mpira wa Bongo hususan uhamasichaji na umecreate GOODWILL ya club ya Simba. Hongera sana Mola akupe afya njema wewe na Familiya yako. SIMBA OYEE

    ReplyDelete
  3. Manara dharau/maneno mengi, Creativity ipi mpya anayoifanya ambayo haipo duniani?
    Sasa ange gundua platform kama za iphone au android applications ange jiita nani?
    Wacha watu wakusifu sio kujisifu na kuponda wengine.

    ReplyDelete
  4. Creativity yako ni kuwaletea mikia chopper? Au kununua mechi ili babu zako washinde uwanjani? Huo u MC ndio jambo kubwa? Natamani uendelee kuandika kiswahili mataifa mengine wasielewe.

    ReplyDelete
  5. Huyu mpiga porojo tu na anaona donge Yanga kufanya makubwa jana na alisema hawana uwezo wa kujaza uwanja na kufanyabusajili. Tatizo ni mnafiki na ndio maana kila siku anatafuta namna ya kujitetea kwa lugha anuai. Anaapa na kutoa ahadi za uongo ambazo badae anageuza maneno na kujidai hakuwa na lengo hilo. Ameshazoea kusimulia porojo zake kwa Wanasimba wenzake wasiojitambua. Kama kweli ameufanyia makubwa mpira wa Tz mbona anashindwa japo kupongeza Azam na Yanga kwa usajili mpya walioufanya? Huyu ni mbulula kabisa kama mambulula wengine tu. Naomba tumpuuze

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anayewajazia uwanja yanga ni manara kwani huwa anawafanyia promo kisiri muda ukifika ukweli utajulikana

      Delete
    2. Yeye mwenyewe kafanya promo kwake na kashindwa kuujaza uwanja; atatufanyiaje promo Yanga?

      Delete
    3. Ukweli usemwe - viingilio vya chini ndiyo vimejaza uwanja siku ya kilele cha wananchi. Kingine ni mashabiki walipoingia bure kwa kusukuma geti na walinxi wakashindwa kuwazuia

      Delete
  6. Mimi huo naona ni sehemu tuu ya utani wa jadi, watu wasitumie nguvu kujibiana. Povu ruksa.

    ReplyDelete
  7. Na ndio creativity yenyewe. Ha ha ha ha

    ReplyDelete
  8. Wakuja utawajua tu.Ba comment zao.Urani wa jadi wa kizazi hiki ni tatuzo hasa. Sunday Manara Mkwe wake alikuwa Mwenyekiti wa Simba .Akazaliwa Haji. Utan huu ni vizazi na vizazi. Wakuja msiugeuze uadui.

    ReplyDelete
  9. Heshima utazipata kwa mke wako na watoto wako na hao wehu wenzio wasijitambua kama wewe

    ReplyDelete
  10. Wacheni matusi ya kitoto. Kama haikuhusu pita mbali. Huhitaji kuonyesha ujahili wako.

    ReplyDelete
  11. Hapa manara umechemka wa kina nugaz wamekupiga bao inatawakiwa uanze kwanza kuwapa heshima yao kwa namna walivyofanya jambo lao jana na lilivyofaana na kwa kuujaza uwanja wa mkapa na pia inatakiwa uige/uchukue yaliyo bora suala la kuwa mhamasishaji bora wa club wa ya simba hilo halina ubishi kila mmoja analijua na simba walikupa tuzo yako. Labda tuzo ya heshima tumpe mo dejwi kwa uwekezaji wake ndani ya club ya simba maana bila yeye bado neno la wamatopeni lingeendelea kushine

    ReplyDelete
  12. Watu wanakubeza tuu lakini taifa linatambua mchango wako katika uhamasishaji

    ReplyDelete
  13. Haji watu watakuheshimu tu endapo utajitengenezea hiyo heshima. Miongoni mwa vitu vinavyoondoa heshma ya mtu ni "mdomo"; kauli. Kauli zako nyingi hasa katika harakati za kutafuta umaarufu, huwa tata sana@
    Wiki iliyopita ulisema "endapo wengine wataujaza uwanja, utatembea kwa miguu hadi Japan"!
    Ahadi ni uungwana; ni zaidi ya deni. Muungwana hutakiwa kutimiza ahadi na viapo vyake. Asiye tekeleza huitwa mbabaishaji, hupunguza heshima yake na haaminiki tena.
    Sijui kwa sasa umefika wapi ukitembea kwa mguu kwenda Japan?

    ReplyDelete
  14. Kuna mstari haji amesema labda kesho itazungumzia anguko la commandoo wa kimakonde lakini behind it kuna kazi kubwa imefanyika"" am agree with it kwani kama diamond ni shabiki la simba na yeye ndo amemtoa konde baasi ni wazi damu ya diamond wasaf group ndio imekwenda kufanya kazi ya kusherehesha siku ya wananchi..yaan mmoja anamchukua baba mwingine ana mchukua mtoto afu unajidanganya watu tofaut wa ka ti vinasaba vya idea ni full complete ivo unaweza sema akili za simba(diamond)ndizo zimetumika kwa wana yanga(harmonize)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic