JUMA Nyangi, nyota wa zamani wa Klabu ya Alliance FC ya Mwanza anatimiza idadi ya nyota sita waliosajiliwa na Klabu ya Mtibwa Sugar.
Nyangi alitambulishwa rasmi jana, Agosti 30 kwa kusaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha wakata miwa cha Morogoro.
Wachezaji wengine ambao tayari Mtibwa Sugar imemalizana nao ni pamoja na Abal Kassim kutoka Azam FC, Baraka Majogoro kutoka Polisi Tanzania, George Makanga kutoka Namungo,Hassan Kessy kutoka Nkana FC na Geoffrey Luseke kutoka kutoka Alliance.
Mtibwa Sugar ilimtambulisha jana Kessy ambaye ni beki wa kulia kwenda kuziba pengo la Shomari Kibwana aliyeibukia ndani ya Yanga.
Nyota hao wataanza kuitumikia Mtibwa Sugar ndani ya msimu wa 2020/21 unaotarajiwa kuanza Septemba 6 kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila.
0 COMMENTS:
Post a Comment