August 27, 2020

 


AZAM FC leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Klabu ya KMC.

Bao la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa na mshambuliaji wao ingizo jipya, Prince Dube dakika ya 89 kwa pasi ya mshambuliaji wao mwingine Obrey Chirwa.

Mchezo wa leo wa kirafiki ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ulikuwa na malengo ya kunoa makali ya timu zote mbili kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.


Timu zote zinakuwa zimecheza jumla ya mechi mbili za kirafiki hivi karibuni ambapo Azam FC ilianza na Namungo FC na ilishinda kwa mabao 2-1 ilikuwa ni kwenye kilele cha Azam Festival.


KMC jana, ilicheza na Simba, Uwanja wa Uhuru mchezo wa kirafiki na ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

1 COMMENTS:

  1. Tulitazamia Azam wapate magoli mengi kwakuwa KMC waliingia uwanjani wachofu kwakuwa Jana yake walikuwa na kibaruwa kigumu dhidi ta Simba, lakini juu ya hivo Azam walionesha soka Safi na lakuvutia. Kila la heri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic