August 28, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Mtanange huo ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa msimu wa 2020/21 ambapo unatarajiwa kupigwa Agosti 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha


Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini watakutana na timu kubwa hivyo watapambana.


 “Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba.Wanatambua kwamba haitakuwa kazi rahisi ila wapo tayari hivyo kilichobaki ni wakati kukamilisha yale ambayo wamejifunza.


"Tunacheza na timu kubwa, wana taji la ligi pia tulikutana kwenye Kombe la Shirikisho tukapoteza hivyo yote ninakumbuka bado sijasahau" amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic