August 27, 2020


 KLABU ya Yanga imebadilisha uamuzi wa kuendelea na kocha Cedric Kaze ambaye alitarajiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

 

Kaze awali ilisemekana amemalizana na Yanga amekuwa akiripotiwa kuja nchini kuandaa kikosi cha Yanga kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi inayofikia kilele Agosti 30, 2020 ambapo watacheza na Aigle Noir ya Burundi, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema Kaze ameomba udhuru wa kuchelewa kuja kutokana na matatizo ya kifamilia.


“Kocha Kaze ametuma ujumbe akiomba wiki tatu zaidi kutokana na matatizo hayo, hivyo uongozi umeona ni vyema utafuta kocha mwingine kutoka kwenye orodha ya waliokuwa wameleta maombi awali haraka iwezekanavyo” imeeleza taarifa hiyo.


Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kuingia kwenye hesabu za Yanga ni pamoja na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omong pamoja Kocha Mkuu wa Taifa Stras, Ettiene Ndayiragije.


Kwa sasa Yanga inaendelea na maandalizi kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

4 COMMENTS:

  1. Mimi ni Yanga wa damu, lakini ninavoiona mimi na huku siku za tulichokipanda kinakaribia wakati wake, viongozi hawaoni wala hawasikii wao wanadelea tu kuyalilia maji yaliyokwisha kumwaika ambayo hayazoleki tena. Morrison hatutaki na hela mliyompa keshakurejesheeni na huko alipo keshahalalishwa na nyie mmo tu. Tunaumia ni sisi mashabiki na mengi yatatutoka na wengine ndio wataofurahi. Jituluzeni jamaa tuvune tulichopanda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi vitendo vya kuharibiana timu kwa kudaka wachezaji kijanjajanja ni bora vikomeshwe. Timu inataka mchezaji ikae mezani na timu husika yapite makubaliano halali mchezaji aende kisheria.
      Mimi naunga mkono yanga katika kutafuta haki yao ili vitendo hivi vya kipuuzi vikome kwenye soka la Tanzania. Kutokana na ujanja ujanja mwingi kwenye soka la Tanzania ndio maana nchi kwenye mechi za kimataifa haifanyi vyema.

      Delete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Yanga Majanga katika miaka ya hivi karibuni. Kwa kifupi tu hakuna njia ya mkato ili kuwa bora. Yanga kuna tatizo la uongozi pale na huo ndio ukweli. Katika mpira wa miguu kocha ndio kila kitu asikuambie mtu leo Yanga wanadiriki kufanya uasjili wa kishindo bila kocha. Nadhani kitendo hiki hiki angekifanya Simba basi vyombo vya habari vingejaa maneno ya shombo juu yao hasa kutoka kwa wale wanaojifanya wachambuzi makocha wakeretwa wa soka nchini,unafiki mtupu.kwanini tusijikumbushe simba walivyoachana na kocha wao na bila ya kuchelewa wakamleta kocha mwengine licha yakuwa na kikosi cha wachezaji wa simba karibu ni kile kile karibu miaka mitatu au minne. Yanga wamesaini karibu wachezaji wote wapya na kocha mpya ambae wachezaji sio pendekezo lake hata kama wachezaji hao wanaonekana wa viwango lakini mchezaji wa kiwango bila kocha ni sawa na gari la samani lisilokuwa na Dereva makini ila yetu macho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic