August 22, 2020


KOCHA wa Inter Milan, Antonio Conte usiku wa kuamkia leo Uwanja wa RheinEnergieStadion aliambulia kadi ya njano wakati timu yake ya Inter Milan ikipoteza taji la Europa League mbele ya Sevilla kwa kukubali kichapo cha mabao 3-2.

Conte alionyeshwa kadi hiyo ya njano baada ya kuingia kwenye mzozo na nyota wa timu ya Sevilla, Ever Banega baada ya kujibizana kuhusu masuala ya nywele. Conte alisikika na mwamuzi wa kati akisema kuwa nitakuona baada ya mechi jambo lililopelekea aonyeshwe kadi ya njano huku neno la Banega aliyemtania kuhusu nywele zake hilo mwamuzi hakuskia.

Sevilla inamshukuru nyota wa Inter Milan, Romelu Lukaku kwa kujifunga goli lililowapa ushindi kwani ngoma ilikuwa 2-2 mpaka dakika ya 72 jambo lililoongeza ushindani kwa timu zote mbili.


Mabao ya Inter Milan yalifungwa na Lukaku mwenyewe dakika ya 5 kwa penalti na Diego Godin dakika ya 35 huku yale ya Sevilla yakifungwa na Luuk de Jung dakika ya 12 na 33 na lile la ushindi la kujifunga Lukaku ilikuwa dakika ya 74.

 Kupoteza kwa Inter Milan pia kunaiweka kwenye hatihati nafasi ya Conte ndani ya kikosi chake cha Milan kwa kuwa inaelezwa kuwa aliambiwa akishindwa kumaliza msimu na taji lolote safari ya kuondoka inamhusu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic