August 16, 2020

 

MSEMAJI wa Simba SC, Haji Manara, leo Agosti 16, 2020 akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Simba, Msimbazi jijini Dar es Salaam, amesema ataomba kupumzika kidogo kutokana na afya yake kutokuwa sawasawa.



“Afya yangu siyo sawasawa madhubuti labda mnaweza mkashangaa…Nisiwakwaze, mnaweza mkashangaa baada ya muda mchache ujao nikawaomba kupumzika na nitumie furusa hii kuwaambia nipo Simba nitawaomba Wanasimba nipumzike kidogo kwa sababu ya afya yangu siyo madhubuti sawasawa, nitaendelea kuhamasisha nje ya Simba. Asanteni sana,” -Amesema Haji Manara.

Haji ameyasema hayo baada ya baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba kushiriki dua maalum ya kuiombea klabu hiyo.


19 COMMENTS:

  1. Mwenyezi akujalie Afya Njema

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Utani si kwenye afya ya binadamu mwenzio

      Delete
  3. Tunakuombea duwa Inshallah Mungu akurejeshee siha yako kamili Bila ya kuchelewa irejee siha yako iwe kama ilivokuwa kabla ya maradhi na umrejee kuendelea na jahazi lako kwasababu huwezi Kumtaja Manara Bila kuitaja Simba wala Simba bila ya kumtaja Manara na tumeshuhudia mengi matamu kwa kuwepo Manara kama ilivo Pilau Bila ns chumbari na ndio ilivo Simba na Manara

    ReplyDelete
  4. Binafsi kama shabiki Wa Dar Young Africans nikuombee kwa Mungu upate siha njema ila kama ni kuzuga labda huko hakujawa sawa aaha mtoto wetu sio poaa

    ReplyDelete
  5. Huyo mpumbavu hapo juu na hiyo comment isiyo ya kibinadamu. Mtu anasema anaumwa wewe unaiita zuga.Utakapougua ndio utajua ukweli. Hujafa hujaumbika. Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema Hsji Manara. Amiiin.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jaman usikimbilie kusema tu mpumbafu. Mazingira wakati mwingine yanatia shaka. Kwa namna tulivyomwona siku ya Kiba na Samatta alivyoshuka kwenye gari na Morrison na kumfunga viatu kwa mbwembwe kwa tunavyomfahamu Manara alivyo na akili inatia shaka. Na ukiangalia mazingira ya Simba kwa sasa inawezekana Manara hataki kuwa sehemu ya yatakayotokea. Ukiangalia Simba imeuzwa na hela haijalipwa, walionunua wamebadili LOGO ya timu bila ata kuwauliza wanasimba. Makao makuu ya Club imetelekezwa. Tunarudia Manara kama unaumwa sisi tunakupa pole. Manara ni mjanja sana mimi nampenda sana, Ata ile trh 08 alipogundua hakuna uwezekano wa timu kushinda Manara hakuwa uwanjani. Hii mechi ya pili alijua 100% timu inashinda aliongea sana. Watu hawajui kwa nini kuna marumbano ya kumng'oa coach anayeonekana kufanya vizuri! !! . Wanajua jinsi walivyotumia mbinu kushinda hayo maubingwa.

      Delete
    2. Yani sasa hv mlichobakisha ni kushindana na Simba kwa maneno yani kwa sababu mnajua mpira hamuwezi yani akili zako zilivyokuwa fupi unawezaje kujua unashinda mechi ya mpira Manara ye ni Mungu mpaka ajue kuwa leo anafungwa au anashinda eti Simba imeuzwa, Mwnyekiti ni mshindo msola lakini wenye sauti GSM alafu kwa akili zajko fupi ata kujiuliza hujiulizi kweli Manyani fc

      Delete
  6. Matamshi yake ni ya kukejeli na huyo mwenye kukejeli na kumkejeli mwengine ajuwe ataumbuka na sijui Anahisi Ana sifa gani za kukejeli lakini mara nyingi huwa na sifa ambazo ndio za ujinga na mengineo

    ReplyDelete
  7. WW HUUMWI BANA UMENUSA HARUFU YAKUTIMULIWA.

    ReplyDelete
  8. Yawezekana nae kamfuata C.E.O...
    Allah amjaalie nafuu apone haraka.

    ReplyDelete
  9. Yanga inabidi wasimkejeli lakini wamuheshimu na kumuenzi. Sakata la Kocha Mzungu wao la ubaguzi wake liliamshwa na Manara wakati wao wenyewe walinyamaza kimya na baada ya matamke yake kuelekezwa kwa viongozi ndipo ilipoibuka hisiya na Kocha kutimuliwa na kila mtu ansyajuwa hayo na leo wana midomo ya kumkejeli na ndio sababu kuu ya matokeo yao mengi ya Mikasa isiyokwisha

    ReplyDelete
  10. Aliyekubakiza Simba alikua ni Senzo,nae ametimkia jangwani,umegundua utatimuliwa sasa unajifanya kuumwa,huna lolote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti alyekubakiza Simba alikuwa Senzo huyo senzo kaja Simba kamkuta Manara, kwa ninavyoona ndugu zetu chuki zimekuwa kubwa kwa huyu jamaa nafikiri mnamuombea hata kifo;ila sisi hatushangai kwa sababu tunajua timu iliyoanzishwa kwa lengo la kucheza mpira ilikuwa Simba(timu ya mpira hasa) lakini wenzetu walianzishwa kwa ajili ya kuwaburudisha viongozi wa CCM (timu ya siasa)kwa hiyo wao mpira kwao ni chuki

      Delete
  11. Mimi nafikiri kama anazuga ni yeye, ila sisi tuchukue kauli yake kuwa anaumwa. Kutoka tarehe ya Kiba na Samatta, mobona mtu unakutana naye asubuhi na jioni unaambiwa amefariki, kwa hiyo kila mtu anatemmbea na ugonjwa.Unaweza kuwa mzima sasa baada ya saa moja ukaugua. kama anazuga atajijua yeye. Pole Manara Mungu na akuponye urejee kwenye hali ya kawaida.

    ReplyDelete
  12. Manara unataka kukimbia bomu bado kidogo linalipuka hapo msimbazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dua la kuku halimpati mwewe mtasubiri sana sisi sio manyani fc

      Delete
  13. Anazuga huyo manara ameshajua hapo Simba hamna kitu anakimbia kijanja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akikimbia wewe inakuuma nini ulitaka akae Simba mpaka awe anatembelea mkongojo acheni chuki binafsi kwa Manara tunajua manyani fc mnamchukia sana huyo mwana lakini vumilieni mdogo mdogo itawaingia

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic