August 30, 2020

 


MJUMBE wa Kamati ya Usajili wa Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema hawakuwa na mpango kabisa wa kumsajili kiungo mchezeshaji mpya Simba raia wa Zambia, Larry Bwalya huku akisisitiza yeye alimuulizia Clatous Chama kwa meneja wake.

 

Hivi karibuni kuliibuka tetesi za Yanga kuwepo kwenye mipango ya kumsajili Bwalya kabla ya siku chache Simba kuchukua maamuzi ya haraka kufanikisha saini ya nyota huyo.


Kiungo huyo amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga hapo akitokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika huko.

 

Akizungumza jijini Dar jana, Hersi alisema kuwa meneja wa Chama ndiye anayemsimamia Bwalya ambaye yeye alifanya mawasiliano naye kumuuliza kama kuna uwezekano wa kumpata Chama.

 

“Meneja wa Chama ndiye huyo wa Bwalya, mimi nilichofanya kumuulizia Chama nikionyesha nia ya kumsajili, lakini sasa kilichotokea ni meneja huyo kuwapigia simu viongozi wa Simba kwa ajili ya kuwajaza.

 

“Meneja huyo aliwapigia simu Simba kwa kuwaambia kuwa, Yanga wameonyesha nia ya kumsajili Bwalya kwa lengo la kuwaongezea kasi viongozi hao ili kukamilisha dili hilo la usajili haraka.

 

“Huyo Bwalya hatukuwa katika mipango naye kabisa, Chama kweli lakini siyo huyo kiungo, nikuhakikishie kuwa Yanga tukihitaji jambo letu hivi hakuna wa kulizuia kama tulivyoamua kwa Mwamnyeto (Bakari) kumsajili.

 

“Tunafahamu moja ya klabu kubwa ambayo pinzani (Simba) ilikuwa ikitangaza kuwa Mwamnyeto ndiye mchezaji wao, lakini mwisho wa siku amekuja Yanga,” amesema.

5 COMMENTS:

  1. Jamaa anajikosha baada ta kumkosa Bwalya.Hata alitoa tweet ya kulalamika.

    ReplyDelete
  2. Kuna kesi ya Mwakalebela kutaka kumsajili chama bila kufata taratibu akadai anatania leo mtu wao anaongea alienda kwa meneja wa chama na kutaka kumsajili chama na hali wanajua ana mkataba hii inaonyesha yanga hawafati sheria na tff inawalea tu lakini wao kila siku ni kulialia tff kwamba wanawabeba simba

    ReplyDelete
  3. Mnaweza kuwabeza SimbaSC kumsajili Larry Bwalya mkaona kama mmewapeleka choo cha kike kumbe mmewapiga teke kuwaongezea mwendo....

    ReplyDelete
  4. Yanga buana! Hivi kuna timu gani hapa nchini inaweza ikathubutu kusema haimuhitaji Larry Bwalya halafu ikamuhitaji Haruna Niyonzima?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic