August 30, 2020


 LEO Agosti 30, Simba inashuka Uwanja wa Amri Sheikh Abeid kumenyana na Klabu ya Namungo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa majira ya 9:00 alasiri.


Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba sita.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck inatarajiwa kukosa huduma ya nyota wake wa kikosi cha kwanza wanne kutokana na sababu mbalimbali kwa mujibu wa kocha mwenyewe ambao ni:-

Beki wa kati raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa.


Luis Miqussone kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji.


Gerson Fraga kiungo mkabaji raia wa Brazili na Chris Mugalu yeye ni mshambuliaji.


3 COMMENTS:

  1. umeshidwa kuandika habar za yanga unaandika za simba achani unazi

    ReplyDelete
  2. Yanga kuna habari gani. BONANZA, hii ndo mechi ya heshima,mechi ya kufungulia ligi. Gongowazi bwana iandikeni kwenye blog zenu

    ReplyDelete
  3. Yanga kuna habari gani. BONANZA, hii ndo mechi ya heshima,mechi ya kufungulia ligi. Gongowazi bwana iandikeni kwenye blog zenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic