August 22, 2020

 KESHO Agosti 23 itapigwa fainali ya kibabe kati ya mabingwa wa Ufaransa PSG dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.


Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili unatarajiwa kupigwa majira ya saa 4 usiku.

 PSG ilitinga hatua ya fainali kwa kuitungua RB Leipzing mabao 3-0 huku Bayern Munich nao wakiwatungua Lyon mabao hayohayo matatu.


Kwenye Uwanja wa ‘Estadio Da Luz’ jijini Lisbon, Ureno miamba hiyo miwili inatarajiwa kukutana.


Timu zote zinasaka rekodi zao kwani ikitokea Bayern Munich ikatwaa ubingwa itaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kutwaa taji hilo bila kupoteza mchezo wowote huku PSG ikiwa itatwaa ubingwa huo itakuwa ni mara yake ya kwanza.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic