August 22, 2020


SENZO Mbata, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, leo Agosti 22 ameibuka ndani ya Uwanja wa Chuo cha Sheria kuwaona wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya wiki ya Wananchi pamoja na Ligi Kuu Bara.


Yanga ilianza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2020/21 Agosti 10 na mchezo wake wa kwanza kwenye ligi unatarajiwa kuwa Septemba 6 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa. 


Senzo amesema kuwa hakuwa na furaha ndani ya timu yake ya zamani ya Simba jambo lililomfanya aibukie kwa watani zake wa jadi ambao  leo Agosti 22 wana jambo lao Uwanja wa Mkapa.


Baada ya kufika mazoezini leo kwa mara ya kwanza, Mbatha alikutana na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa msimu huu kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko ambao walipokolewa kifalme Agosti 20 walipotua Bongo.


Nyota hao wawili wamemalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili wakitokea AS Vita wanapewa nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa wameahidi kupambana kutimiza malengo waliyojiwekea.

 Nyota wote wapya wa Yanga wanatarajiwa kutangazwa Agosti 30 kwenye kilele cha siku ya Wananchi ambapo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambapo timu ya Rayorn Sports inatajwa kutua kucheza na Yanga. 

6 COMMENTS:

  1. Etii hakua na furaha,usiache mbachao kwa msala upitao...

    All the best!

    ReplyDelete
  2. Hivi yanga wanacheo kinaitwa "Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba"!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. duuh!!!!.....sio bure,mimi ni shabiki wa simba lakini huyu jamaa inaonekana hata darasa la kwanza hajaliona......hawa ndio wanaotufanya wana simba wote tuonekane mambumbumbu.

      Delete
  3. Wewe mkia Elimu inakuponza jiongeze unapoongea na Wanaumme

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic