August 22, 2020

 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpango mkubwa kwenye kilele cha Wiki ya Wanachi, Agosti 30 ilikuwa ni kucheza dhidi ya Klabu ya Sevila ambao ni mabingwa wa Kombe la Europa League baada ya kuwatungua mabao 3-2 Inter Milan kwenye fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa walikuwa wanahitaji kucheza na Sevilla siku ya kilele kwa kuwa  wanaushirikiano nao mkubwa ila mipango imekwama.

"Timu yetu ya kwanza ambayo ilikuwa ni chaguo letu kucheza nao ilikuwa ni Sevilla kwa kuwa tupo nao kwenye ushirikiano lakini mambo yamekuwa magumu kwa kuwa janga la Virusi vya Corona limevuruga mambo mengi na imekuwa ngumu kwa sasa kupata timu ambazo zinaweza kuwa huru kwenye kusafiri.

"Tuna uwezo kwa kuwa Yanga ni timu kubwa na inafanya mambo makubwa, tunaongoza kwa kuwa na mataji mengi hivyo hatuna cha kuhofia. Kwa kuwa tumeshindwa kuwapata Sevilla bado tunaendelea kufanya mawasiliano na timu nyingine ili tuweze kucheza mchezo mzuri wa kimataifa Uwanja wa Mkapa.

"Tutaitangaza timu ambayo tutacheza nayo hivi karibuni ila kwa sasa tumetuma barua pia kwa Rayon Sports ya Burundi nayo ni timu kubwa mipango ikikamilika kila kitu kitatangazwa," amesema.

14 COMMENTS:

  1. Rayon Ya Burundi? Timu Kwanza haina kocha wachezaji nao bado wengine hawajafika mazoezini hamjui mfumo gani mnacheza halafu mnataka mcheze na Sevila, Wenyewe Sevila kwa Tz wanajua Simba Tuu Ndio tuliwatoa jasho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sevilla walikuja kutalii nyie mkatoa macho ndio maana mwishoni wakatumia dk 10 kuwafunga goli 3

      Delete
    2. Ata mi nawashangaa sana yanga

      Delete
  2. Mmmmm! Tuwe wakweli, mcheze na sevila kwa timu ipi. Hii ya kuunga unga? Watu wengine wamepokelewa jana na wengi mliwatema sasa mtawezaje kutengeneza mfumo ktk kipindi cha wiki moja hadi kucheza na sevila? Mnataka kutuletea aibu tuu kama taifa.

    ReplyDelete
  3. Hawa wanafikiria kuingia level ya simba ndio maana baada ya simba sumtoa jasho Sevilla harakaharaka wakaunga urafiki vita alivyomfunga simba mechi ya kwanza wakaunga naye urafiki kiukweli hawana cha zaidi ya utopolo

    ReplyDelete
  4. Yaani umefungwa bado unajisifia umewatowa jasho
    Ama kweli bora ukose mali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaona ajabu simba kufungwa na Bingwa wa kihistoria wa Europa? Sidhani kama mpira unaujua

      Delete
  5. Mlijaribu kuwatekenya halafu mkaifyetuwa mbio kukimbilia mitini. Kwanini Mnyama akapata timu ya kujima mkaikosa nyie. Tupeni ukweli Bwanaaa

    ReplyDelete
  6. Hilo ndilo tatizo la kujifunzia ukubwani kushabikia mipira mnashindwa kujenga hoja mnaongelea ujinga tu Simba inanikipya hasa ambacho wengine hawana miaka yote ilikuwa wapi kama walivyojiandaa wao na wengine wanaweza pia kuleni kande mkalale watoto wa mama sawa

    ReplyDelete
  7. Utopolo mnajikosha eti Sevilla baada ya kusikia mnyama tuliiihitaji kucheza na alhaly nanyi mwajikosha

    ReplyDelete
  8. Sevilia hawakuja wameona aibu timu yenye utukufu wake Kutoka bara la Ulaya kupoteza wakati kwenda kucheza na timu di kiasi chao, si corona wala lolote

    ReplyDelete
  9. Hao wa nasikia wazungu wa nasikia tu sifa za nchi yetu na jinsi watalii wanavomiminika ns kujionea ikiwemo mbuga za wanyama pori na ukarimu wa watu wake, lakini sio kucheza mpira ns kucheza na timu inayochapwa ovyo ovyo

    ReplyDelete
  10. Mnyama aendelea kufanya yake utopolo povu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic