August 26, 2020


 NYOTA mwingine wa Yanga ambaye yeye ni mshambuliaji anatarajiwa kutua leo Agosti 26 ili kujiunga na wachezaji wenzake ambao tayari wameshaanza mazoezi.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso ni mshambuliaji anaitwa Yacouba Sogne na tayari alishamalizana na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili.

Wengine ambao ni washambuliaji waliomalizana na Yanga ni pamoja na Michael Sarpong raia wa Ghana na Wazir Junior yeye ni mzawa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota huyo alikuwa na udhuru kutokana na 'lockdown'.

"Lockdown ambayo imesababishwa na janga la Virusi vya Corona ilikuwa inaendelea nchini kwao na ilifanya ashindwe kuja ila kwa sasa imeshaisha na tunatarajia anaweza kutua leo ili kuungana na wachezaji wenzake," emesema.

6 COMMENTS:

  1. Wanajipya? Ukiwa bingwa Wa kukosoa kubali kukosolewa. Mikia bwana hawana jema ila kwa kuwa Moira ni uwanjani tukutane huko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaongea uku unatetemeka sisi sio watu wa kucheka cheka imbeni taarabu lakini tunajua tarehe 18 sio mbali, mnatafanya usaijili mwingine upya maana akili zenu zinavyowatuma kuwa mshapata dawa ya simba ila kinachoenda kuwakuta wenyewe wanasema tutazidi kuwakera

      Delete
  2. Vibaka sc ,mnampora mpaka bosi wenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic