August 26, 2020

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck akishirikiana na Selaman Matola, leo Agosti 26  kitacheza mechi mbili za kirafiki.

Itacheza dhidi ya KMC na Transit Camp Uwanja wa Uhuru na itakosa huduma ya mshambuliaji wao mpya, Chris Mugalu raia wa Congo ingizo jipya kutoka Lusaka Dynamos ambaye jana alisepa kuelekea nchini Congo.

Mechi hizi mbili ni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 30, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha dhidi ya Namungo pamoja na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ligi inatarajiwa kuanza Septemba 6 ambapo Simba mchezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Ihefu, pale Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

2 COMMENTS:

  1. Kasepa ndio basi harudi tena au?

    ReplyDelete
  2. Toa taarifa inayo jitosheleza mwandishi,Mugalu kasepa atarejea tena au ndo basi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic