August 31, 2020

 


ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Yanga kuachana na mvutano wa suala la mchezaji, Bernard Morrison kwa kuwa wanapoteza muda na badala yake wawekeze nguvu kuibua vipaji vipya.


Kikwete ameyasema hayo jana, Agosti 30 kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi ampabo yeye alikuwa ni mgeni rasmi Uwanja wa Mkapa.

Morrison amekuwa kwenye mvutano na Yanga kuhusu suala la mkataba, Yanga inaeleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili huku Morrison akisema dili lake la miezi sita lilikwisha.


Shauri hilo lilisikilizwa Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji Tanzania kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 na mwisho Morrison alitangazwa kuwa mshindi kwa kile kilichoelezwa kuwa kulikuwa na mapungufu kwenye mkataba.


Kikwete amesema:"Naskika ninyi mwaka huu mmeibiwa mchezaji na majirani zenu,hilo ni jambo la kawaida kwani masuala haya kwa watani wa jadi hayajaanza leo ni tangu zamani yalikuwepo haya masuala.


"Kwa kuwa ninyi mmeibiwa Morrison najua nanyi mtajipanga wakati mwingine tena mtaiba mchezaji wao mzuri ni kawaida. Lakini naona masuala haya ya kupelekana FIFA ni kupoteza tu muda kwani kuna namna ya kufanya ili kutofikia hatua hiyo.


"Kinachotakiwa ni kuibua vipaji wenyewe ndani ili iwe rahisi kuwapata nyota ndani ya nchi, sasa leo tunagombania mchezaji kutoka nje na pia tumesajili wachezaji kutoka nje hii isingekuwepo kama tungekua tunaibua vipaji vyetu. Tumeona kuna makocha wa kigeni waliletwa hawa wa kuokotaokota matokeo yao yalivyokuwa ilionekana ila simtaji ni nani," amesema.


Agosti 22, Morrison, kilele cha Simba Day, Uwanja wa Mkapa alitambulishwa kuwa mchezaji wa Simba.Agosti 30, kilele cha Wiki ya Mwanachi alitambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga kwa kuwa shauri lake limepelekwa Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo,(Cas).

13 COMMENTS:

  1. Ni ushauri mzuri lakini uliochelewa kwa vile viongozi wa Yanga wameshapeleka shauri lao CAS

    ReplyDelete
  2. Busara za rais mstaafu mwenye akilitinamu na asikie na kuelewà. Ashaona mashabiki wanapigwa Changa lamacho na gsm na viongozi wao wakijua Hamna Chao pale ili kujikosga kwa mashabiki na wanachama ndo wanawadanganya eti CAS

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jifunze kuandika vizuri alafu ndo uje uwaponde GSM

      Delete
  3. Maneno ya Mheshimiwa ni ya busara na ukweli wa hali ya juu, kwani wakati wa enzi ya Manji, watani waliwachomoa wachezaji wengi wa Simba kwa njia mbaya na ya aibu kubwa, walifanya kuliko hayo waliyofanya Simba. Mfano mmoja tu pale Simba walipomleta yule beki Mrundi ambaye walikuwa Simba wameshamtolea gharama kubwa sana, jina lake nimelisahau na pale alipotia mguu tu, sisemi kuwa watani walimuiba lakini nasema wakamuhaijeki na hilo la aibu ni kuwa wakikataa kuwarejeshea Simba haki yao ya gharama waliyotoa na kwa upande wa Simba, Morrison aliwarejeshea Yanga hela yao yote aliyipokea na huo ni uungwana na uaminifu wa hali ya juu na tunataraji wataipokea nasaha ya Mheshimiwa Kikwete baada ya kuzipuuza nyingi za wengineo

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa Yanga bhana tabu kweli kweli. Kwa ushauri huu kumbe itakuwa hawajapeleka kesi yo yote CAS!

    ReplyDelete
  5. Yanga hawawezi kupeleka kesi CAS, kwani hawajitak8? Wanachofanya ni kuwalaghai washabiki wao tuu. Sasa mzee kawaambia ukweli waendelee kushipaza shingo tuone.

    ReplyDelete
  6. Mikia habari ikielemea kuwabeba munasifia azim hakumshari mo kumuacha morisson nyie mulimuunga mkono mzee kashauri au maneno yake hukumu ya cas acheni unafki hata ratiba za ajabu kipindi cha manji zilitokea nyie sio watani munataka tuwe maadui ila yanga niwavumilivu sana hamuchelewi kuvunja viti

    ReplyDelete
    Replies
    1. We nyani F.C watu wanavunja viti kwa sababu ya madudu ya refa uwanjani, mpira sio rede mpira wa miguu unachezwa na miguu na sio mikono labda kwenye mpira wa kurushwa, alafu mlikuwa hamuwezi kuifunga simba mpaka mchezaji wa simba apewe kadi nyekundu ila sisi tunawafunga mpo wote 11 shenziiiiiiiiiiiiiiii!!!

      Delete
  7. utafita wangu unaonyesha ada ya kusikiliza kesi CAS ni dola 15000 hapo ni jaji mmoja majaji wawili ni $30000 sawa na milion 80 za kibongo zingetosha kusajili mchezaji aina ya morson maana kwanza huna hakika ya kushinda pia tena tarehe ya kesi inaweza kwenda mpaka msimu mzima kwa kweli ni kupoteza muda

    ReplyDelete
  8. Hiyo gharama itarudishwa na aliyeshindwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. kupoteza muda...jambo moja la uhakika usajili wa Yanga kwa Morrison una baadhi ya makosa..Yanga wasitegemee kwamba hata wakishinda hakuna kasoro CAS hawatagundua matatizo ya Yanga.Sio kweli kuwa hata wakishinda kutakuwa na faini ya milioni miasita kuelekeea Simba

      Delete
  9. Kikwete kasema hata wao wachomoe mmoja kutoka Simba..Kama huyo beki wanaye jisifia kuwa walimchomoa akiwa anaelekea Simba..inatosha..zingine sasa sifa

    ReplyDelete
  10. Hawa Migongonje ovyo kabisa. Hujipeleka airport kwa makundi eti kuwapokea na kuwashangilia wachezaji na hukaa mpaka jioni ndio hutimuliwa na polisi kurejea makwao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic