August 4, 2020

JEURI ya fedha! Ndivyo utakavyoweza kusema hivi sasa baada ya Kampuni ya GSM kutumia Sh milioni 210 kufanikisha usajili wa wachezaji watatu mfululizo na wakaongeza mtupiaji namba moja ndani ya Mbao FC na kukamilisha idadi ya wachezaji wanne.

Katika usajili huo, mchezaji mmoja, beki Bakari Mwamnyeto, amesaini mkatab, Yanga wakiwazidi ujanja Simba ambao saa chache baada ya kusaini Yanga wakiwa hawajui chochote, walimuwekea ofa ya Sh milioni 180.

GSM inafanya usajili huo kwa kushirikiana na Kamati ya Usajili ya timu hiyo katika kukiimarisha kikosi chao ili msimu ujao wawe tishio na kuwapoka ubingwa watani wao, Simba.

Yanga imemvuta kiungo mkabaji wa Kagera Sugar, Zawadi Mauya, beki wa kati wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto na beki wa kushoto wa Polisi Tanzania, Yassin Mustapha ‘rasta’ huku wachezaji hao watatu ikielezwa kuwa wametumia gharama ya Sh milioni 210 kufanikisha usajili wa nyota hao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa katika hizo Sh mil 210, Mwamnyeto amechukua Sh mil 150 zilizomshawishi staa huyo wa Coastal kumwaga wino Jangwani. Lakini muda mchache baadaye, alipokea simu ya ofa ya Simba ya Sh mil 180 lakini tayari ilikuwa ‘too late’ kwa kuwa alikuwa ameshamwaga wino Jangwani.

Aliongeza kuwa, Mustapha na Mauya kila mmoja amechukua Sh mil 30 na kufikia Sh 60Mil ambazo ukizijumlisha na za Mwamnyeto, zinafikia jumla ya 210 Mil.

“Bado uongozi wa Yanga kwa kushirikina na GSM unaendelea na usajili wao, walianza na usajili wa wachezaji wazawa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja, bado wachezaji kama wawili ili kukamilisha usajili wa wazawa.

“Kwani tayari tumekamilisha usajili wa Mauya, Mustapha na Mwamnyeto ambao wote ni wazawa baada ya kumalizana na hao tunaelekeza nguvu kwa kiungo mshambuliaji mmoja mzawa ambao ndani ya siku hizi mbili utakuwa umekamilika.

“Baada ya hapo nguvu tunazielekeza kwa wachezaji wa kimataifa ambao kuanzia wataanza kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa ajili ya vipimo vya afya na kusaini mikataba.

“Wachezaji wanaotarajiwa kutua siyo majina mageni mdomoni mwa watu kutokana na kati yao kutajwa kwenye Vyombo vya Habari kuwa watajiunga na Yanga kwenye msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, kuzungumzia hilo, alisema: “Mkataba ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, hivyo ni ngumu kutaja dau la usajili la mchezaji.

“Hivi sasa uongozi upo kwenye mipango ya kukisuka kikosi kitakachokuwa imara na tishio kitakachokuwa bingwa kwenye msimu ujao, tayari tumemalizana na Mwamnyeto, Mustapha na Mauya waliokuwa kwenye mipango yetu.”

Nyota wa nne ni Waziri Junior Jr kutoka Mbao FC amejifunga miaka miwili.

Waziri ndiye kinara wa mabao kwenye Klabu ya Mbao akifunga jumla ya mabao 15 katika mashindano yote na kutoa asisti nne. Waziri amefunga mabao 13 kwenye Ligi Kuu Bara na mawili kwenye mashindano ya FA, licha ya timu yake kushuka daraja.


4 COMMENTS:

  1. Yanga ilitakiwa kuanza na usajili wa kocha ndyo aje asimamie usajili, viongozi wanasajili mwisho kocha anakuja na falsafa ambayo wachezaji wachache wanamudu inaanza timua timua tena.

    ReplyDelete
  2. Mwamnyeto sio wa kusajiliwa kwa 180m, ni yanga tuu wanajipoza maumivu ya kuliwa 150m.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa, huyo sio wa bei hiyo

      Delete
    2. kweli kaka hiyo bei ni kubwa sijui waliogopewa nn kwakweli lazima tufikiri kabla ya kutenda huku kuna mabeki tena bora hapo kenya na uganda tena kwa bei ndogo sana maana wanajua TZ soka linalipa. Mwamnyeto wewe sio wa milion 150 Simba wachochea moto weee nyie nao mnajilipua

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic