August 4, 2020


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kama atakuwepo ndani ya kikosi hicho msimu ujao ama hatakuwepo ni lazima ushirikiano uendelee kufanyika kwa uongozi pamoja na wachezaji ili kufikia malengo kwenye michuano ya kimataifa.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho alipokiongoza kikosi chake kushinda mabao 2-1 mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Nelson Mandela, Agosti 2.

Huenda mambo yakabadilika ndani ya Simba kwa kauli ya Sven kwani inaonyesha kuwa hana uhakika wa maisha yake ndani ya kikosi hicho licha ya kwamba ameweza kukiongoza kikosi kutwaa mataji mawili mfululizo ikiwa ni Ligi Kuu Bara pamoja na Shirikisho.

Simba ina tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushinda taji la Ligi Kuu Bara ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema:-"Siwezi kuzungumzia kuhusu masuala ya Ligi ya Mabingwa kwa sababu sijui itakuaje hapo baadaye kama nitakuwa ni mimi ama sitakuepo ndani ya kikosi.

"Lakini ninachofikiria kwa sasa changamoto ya kwanza ni kuweka timu katika umoja na kuweka usawa kwa kila mmoja hili itasaidia kuweza kufikia malengo.

"Furaha yangu ipo kwa timu kutwaa taji la Shirikisho ila niamini mimi kwamba furaha yangu ipo ndani ya moyo," alisema Sven alipokuwa akizungumza na Azam TV.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa uongozi haujasema kwamba umefukuza kocha hivyo taarifa hizo ni za uchonganishi.

1 COMMENTS:

  1. Mwandishi wetu karibu kuandika vizuri, kwa mfano; zungumzia mkataba wake, na vitu Kama hivyo. Na inaonekana wewe usingependa awepo hapo huyo kocha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic