August 22, 2020

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mashabiki wasikose kesho kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Azam Complex kwenye kilele cha Azam Festival.

Agosti 23, Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania ina jambo lao ambalo litakuwa na burudani za kutosha kwa mashabiki wao.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa:" Kwanza tunawaomba watu waje kwa wingi, kutakuwa na jogging, mechi ya timu zetu za vijana, timu yetu itacheza dhidi ya Namungo na msanii maarufu nchini King Kiba naye atakuwepo," amesema.

Ofisa Habati wa Azam FC, Thabith Zakaria amesema kuwa:"Mpira ni wa mashabiki na sio wa klabu, tunaenda kuwatambulisha wachezaji wao kwa ajili ya msimu ujao," amesema.

Pia, Msaga Sumu, naye atakuwepo kwenye Tamasha la Azam FC Festival ndani ya Azam Complex.


Msaga Sumu mbali na kutoa burudani kwa mashabiki watakaojitokeza kwenye tamasha hilo, pia atatambukisha wimbo wake alioitungia Azam FC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic