KLABU ya Azam FC yenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam, jana Agosti 30 ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na Klabu ya Tanzania Prisons.
Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa Uwanja wa Azam Complex na malengo yake makubwa ni kujiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21.
Msimu mpya unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 6 baada ya jana Agosti 30 pazia kufunguliwa rasmi baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kati ya Simba na Namungo.
Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-0 na kusepa na taji la Ngao ya Jamii mbele ya wapinzani wake Namungo.
Azam FC itafungua pazia Septemba 7 kwa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex huku Prisons ikianza na Yanga, Septemba 6,Uwanja wa Mkapa.
0 COMMENTS:
Post a Comment