IMEELEZWA kuwa baada ya Simba kumalizana na usajili wa wachezaji watatu David Kameta, Ibrahim Ame na Charles Ilanfya, timu hiyo haina mpango wa kuongeza usajili wa wachezaji wengine wanaocheza ligi ya ndani.
Inasemekana kuwa uongozi wa Simba umeshakamilisha usajili wa beki wa kulia Kameta kutoka Lipuli, beki Ame kutoka Coastal Union na mshambuliaji Ilanfya kutoka KMC, wote kwa mikataba ya miaka miwili.
Chanzo cha kuaminika ndani ya Simbe kimeeleza kuwa baada ya kumalizana na wachezaji hao Simba haitakuwa na mpango wa kusajili mchezaji mwingine wa ndani na badala yake watageukia usajili wa wachezaji wa kimataifa.
“Simba kwa sasa tutaangalia zaidi usajili wa wachezaji wetu wa kimataifa, kuhusu wachezaji wazawa sidhani kama Simba itaongeza wachezaji wengine, maana hata tulionao unaona jinsi gani wapo kwenye kiwango bora.
“Kitu ambacho kilikuwa kinatufanya tusiweze kufanya mambo mengine ni fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, lakini baada ya kumalizika mambo yatakuwa sawa na tutakuwa kwenye mambo ya usajili,” kilisema chanzo.
Naye Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa: “Simba msimu huu itasajili wachezaji wasiopungua watano ambapo kama tutasajili wawili wa kimataifa basi wazawa watakuwa watatu na kama watatu wakiwa wakimataifa basi wawaili watakuwa wazawa,” alisema Manara.
Almuhim tunaomba Mungu Mtukufu uendelee utulivu na nidhamu ya timu yetu, tupige hatuwa kubwa kimataifa na kuendelea na ubingwa hapa nyumbani kwa msimu ijayo mingi kama tulivofanya msimu mitatu iliyopita
ReplyDelete