MKURUGENZI uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa baada ya kufanikisha usajili wa beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto, sasa unafuata usajili wa kishindo na kihistoria wa wachezaji wa kigeni.
Usajili mwingine wa kishindo ambao wameufanya Yanga ni wa mshambuliaji wa Mbao FC, Waziri Junior ambaye ilidaiwa pia alikuwa akiwaniwa na Simba pamoja na Azam, ambapo Yanga walimpata baada ya kumficha kwenye hoteli kubwa jijini Mwanza muda mfupi baada ya kumalizika mechi ya mwisho ya Mbao FC ya Playoffs dhidi ya Ihefu.
Hersi amesema kabla ya usajili kufungiliwa aliahidi kufanya usajili mkubwa kwa sasa nguvu zao wamezielekeza kwenye usajili wa kimataifa kwa kuhakikisha wanafanya usajili wa kishindo na kuwashtua watani wao wa jadi, Simba waliokuwepo kwenye vita kubwa ya usajili katika msimu ujao.
“Kama unakumbuka vizuri kabla ya usajili mkubwa kufunguliwa nilitoa ahadi ya kufanya usajili wa kishindo na kushtua ambao tayari tumeufanikisha kwa kumsajili Mwamnyeto tuliyekuwa tunamgombea na watani zetu Simba.
“Hivyo baada ya hapo ninaahidi kuwapa sapraizi mashabiki wa Yanga kwa kufanya usajili mkubwa wa kishindo wa mchezaji kutoka nje ya nchi, ninafahamu mashabiki wana hofu kubwa baada ya kuachana na baadhi ya wachezaji.
“Tunachosubiria ni anga za nchi ambazo wachezaji wetu wanatokea ifunguliwe baada ya hapo ndiyo nyota wetu hao wataanza kutua nchini tayari kwa ajili ya kusaini na kujiunga na kambi ya pamoja iliyopangwa kuanza Agosti 10, mwaka huu,” alisema Hersi.
Chanzo: Championi
Katika kikosi bora kilivhotajwa msimu 2019/2020 watani hawakuambulia hata mchezaji mmoja
ReplyDelete