August 21, 2020

 

UONGOZI wa Simba, umesema kuwa sababu kubwa ya kumtimua Patrick Aussems aliyekuwa kocha wa timu ni suala la fedha pamoja kushindwa kufikia malengo ambayo walikuwa wamejiwekea awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,'Mo Dewji' amesema kuwa Aussems maarufu kama uchebe ni kocha mzuri lakini walishindwana naye kwenye makubaliano.

"Tulitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tukiwa na Uchebe ni furaha kwetu lakini tulitolewa kwenye Kombe la Shirikisho mapema hatukupenda.


"Ukiachana na hilo baada ya timu kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu unaofuata tulishindwa kufika mbali na kupoteza nafasi nne kwa taifa hilo nalo lilituumiza kwani tulishindwa kufikia malengo yetu hilo lipo wazi.

"Vile vigezo vyote alivyokuwa anataka tulitimiza kwani mnajua kwamba kulikuwa na mgogoro kati yake na Masoud Djuma ambaye alikuwa ni kipenzi cha mashabiki, tulipokubaliana kwamba aondoke kwa kuwa malengo yalikuwa ni kuona kwamba uchebe hawi na sababu ya kutuambia kuwa hatukumsikiliza.

"Kwa sasa tupo na Sven Vandenbroeck tunaendelea vizuri kwani ameweza kutwaa taji la Shirikisho na Kombe la Ligi Kuu Bara, hivyo bado tuna malengo makubwa ya kufanya vizuri kimataifa, hatupendi kuishia kwa mataji ya ndani hapana," amesema.

13 COMMENTS:

  1. Mwongo umekalia kununua mechi. Unaua mpira wa Tanzania. Unaona wachezaji wako akina Boko hawana msaada kwa timu ya Taifa kwa sababu ya kuwanunulia mechi.

    ReplyDelete
  2. Tatizo kimataifa mecho hazinunuliki, zaidi ya hapo ni hamsahamsa tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo mnazingua, ninyi msiyonunua mechi npo wapi? bongo chali, mapinduzi chali,sport pesa chali, tukawabeba kimataifa chali. Yetu macho mmesajili team mpya tuone mbwembwe zenu uwanjani.

      Delete
  3. Hivi ile 4G ilinunuliwa bei gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani asiyejua kuwa mlimnunua Shishbaby na mwizi wa magari?

      Delete
    2. Shiboub kawashinda, mmeenda kuokota magarasa nje hko, na kuishia kunyanyua vibopa Kama wanafunzi wa primary

      Delete
    3. Shiboub katushindaje, mchezaji gani wa simba ameachwa na alikuwa kwenye kikosi cha kwanza? Kwa namna nyingine Simba imesajili sub kwa sababu kikosi kizima bado kipo.

      Delete
  4. Yanga ni shida,hata kwenye ulweli haeakubali, wanakomaa na porojo za viongozi wao

    ReplyDelete
  5. Huyu brother Mimi nimesema toka mwanzo yupo sawa ,nadhani alikuwa anajibu swali , sasa Mr Salehe Ally wengine mtuelewe kuhusu Haji Manara .Kwenye Redio nadhani EFM au WASAFI aliongea almost saa nzima anaulizwa na hakina Maulid Kitenge alisema inshort yule Coach Ni Agent alitaka kuwapiga Tena akasema hata zile mechi za Hamsa kwenye CAF Champion League no zake ,na walizo shinda hapa was wanajua walishindaje.Anaitwa Msemaji wa Simba

    ReplyDelete
  6. Haji mbona anaongea tofauti na kebehi juu au tumpime utimamu wake. thanks

    ReplyDelete
  7. Kiukweli mnafiikiri simba tuna uwezo wa kuwahonga wachezaji wa As Vita, Al Ahly? Kama Al Ahly Mchezaji wao mmoja tu tunasajili kikosi nusu cha simba. Lakini kukubali kuwa tuliwafunga uwanjani hamtaki mnakimbilia simba kanunua mechi. Utopolo ni shida yaani hadi mawazo ni ya kufoji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic