BAADA ya kumshusha leo mchezaji mpya Michael Sarpong, raia wa Ghana ili kuja kumalizana na Yanga kwa ajili ya msimu wa 2020/21. Uongozi wa Yanga umesema kuwa unafanya usajili makini kwa manufaa ya timu na wachezaji.
Leo Agosti 21, Sarpong ameshuka Dar kwa ajili ya kukamilisha usajili wake ndani ya Yanga na habari zinaeleza kuwa ni dili la miaka miwili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wana imani siku ya kilele cha wananchi Agosti 30 watakuwa na wachezaji wengi wazuri ambao watapambana kwa ajili ya msimu ujao.
"Tupo kwenye maboresho ya kikosi chetu ndio maana unaona usajili wetu tunaufanya kwa umakini mkubwa na kuweza kufanya mambo kwa usahihi imani yangu ni kwamba kila mmoja atafurahi kuona yale ambayo tunayafanya.
"Mashabiki wasiwe na mashaka waendelee kutupa sapoti na wiki ya Wananchi tunaanzia makao makuu ya nchi Dodoma kisha tutamaliza ndani ya Uwanja wa Mkapa, wote tupo tayari na tunapenda kufanya mambo mazuri," amesema.
Sarpong amesema kuwa anafuraha kubwa kwa kuwa amepokewa na mashabiki kwa furaha jambo ambalo ni deni kwake.
Pamoja na furaha na Uyanga wangu ,hivi hao jamaa Team ipo Songea wapo, Uwanja wa ndege wapo naona hata Simba vile vile sura Kama hizo za kujirudia zipo je wanalipwa au wanajitolea majibu anayeuza
ReplyDeleteAnayeuza/anayejua nilimaaniasha
ReplyDeleteKwa soko letu bongo, usajili unatrend zaidi ya ligi yenyewe
ReplyDeleteAya bhna
ReplyDeleteSisemi Hersi nasema hao wawili wenye jezi za Yanga
ReplyDeleteHatutaki neno la kibabe lisilo na tija lakini tunataka magoli ya kibabe
ReplyDelete