September 1, 2020

 


Beki wa kati Gabriel dos Santos Magalhaes amemalizana na Klabu ya Arsenal na amepewa jezi namba sita.


Beki huyo mwenye miaka 22 ni raia wa Brazil amejiunga na Klabu ya Arsenal akitokea Klabu ya Dinamo Zagreb alikopelekwa kwa mkopo msimu wa 2018 pia alicheza Troyes kwa mkopo msimu wa 2017/18 akitokea Klabu ya Lille.


Kwa msimu wa 2018 akiwa ndani ya Dinamo Zagreb alicheza jumla ya mechi 10.


Kocha Mkuu wa Arsenal,  Mikel Arteta amesema kuwa mchezaji huyo yupo imara na ataongeza nguvu ndani ya timu yake.


"Karibu sana  Gabriel ndani ya Arstica. Ni mchezaji mwenye ubora na imara ndani ya uwanja alithibitisha hilo akiwa ndani ya Lille tunaamini atakuwa imara ndani ya Arsenal, " amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic