JUMA Nyosso, mkongwe ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao atakipiga ndani ya Klabu ya Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.
Nyosso alikuwa nahodha ndani ya Kagera Sugar msimu wa 2019/20 mkataba wake uliisha ndani ya timu hiyo na mabosi hawakumuongezea mkataba mpya.
Habari zinaeleza kuwa tayari kwa sasa ameshamalizana na Ruvu Shooting akiwa ni mchezaji huru.
"Nyosso kwa sasa ni mali ya Ruvu Shooting kwa kuwa mkataba wake ndani ya Kagera Sugar ulikwisha hivyo ameingia ndani akiwa ni mchezaji huru na ataendelea kuwa ndani ya ligi msimu wa 2020/21." alisema mtu wake wa karibu.
Atacheza team zote bongo
ReplyDeleteWachezaji wetu wa Yanga wajibidiishe sana kwenye ukabaji. Mwamnyeto naye asiwe mzembe nyuma kufanya chenga ilitugharimu na Ruvu shooting
ReplyDelete