September 28, 2020

 


BEKI wa kati wa Yanga, Lamine Moro raia wa Ghana, ameshindwa kujizuia na kutamka waziwazi kuwa Simba msimu huu wana beki nzuri.

 

Moro ambaye amejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Buildcon FC ya Zambia, msimu huu mpaka sasa amecheza mechi tatu na kufunga mabao mawili kwenye ligi.


Safu ya ulinzi ya Simba inaundwa na Pascal Wawa, Kennedy Juma, Joash Onyango, Ibrahim Ame, David Kameta, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael na Erasto Nyoni.


Kwa upande wa walinzi wa Yanga msimu huu ni Moro, Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma Makapu, Kibwana Shomary, Adeyum Saleh na Paul Godfrey.

 

Moro amesema pamoja na kuwa kikosi chao ni kizuri lakini safu ya ulinzi ya Simba ina ubora mkubwa msimu huu kuliko timu zingine ligi kuu.

 

“Mimi sipendi uongo, mabeki wote wa timu ya Simba wako vizuri hata kama sio timu yangu ila nasema ukweli kuwa Simba wana mabeki wazuri na wenye viwango vya juu,” amesema Moro.



Chanzo:Championi

7 COMMENTS:

  1. Acheni uongo bumbu nyie alisema wapi... yani nyie na kiblog uch**ra waongo

    ReplyDelete
  2. Kataa ukweli mpaka utapodhihirika.Lamine Moro kahojiwa na Globalpublishers. Ba akayasema hayo.
    Mimi ni Yanga lakini inatia aibu baadhi ya wapenzi wetu kutoheshimu rai za watu wengine.
    Je mtu akisema kesho ni jumanne utapinga tu kwa sababu hupendi kukubali kwamba kesho ni jumanne?
    Tuache ushamba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alihojiwa akiwa kambini au? Mbona global hwajaiweka video yake kwenye page yao. Usitudanganye

      Delete
    2. Hajawahi kuhojiwa na chombo chochote huo muda ataupata wapi? kanuni zinawabana sasa hivi mambo yamebadilika Yanga inaendeshwa kiprofessional hakuna mijadala na vyombo vya habari hovyo hovyo

      Delete
  3. Ila hili gazet linapoteza mvuto kw wasomaji wke cjui mwalili wa gazet hili anakubar vpi upuuz huu ni Lina na wpi huyo mchezaji alifanya hayo mahojiano hzi cku tatu mpka nne toka jna timu IPO kambin wpi aliyafanya hayo mahojiano!? Mkela sna na habar za kupandikiza jitafkalina sna mnafanya kz nzur sna ya kutuletea habar lakin mnafeli pakubwa kw uandishi huu

    ReplyDelete
    Replies
    1. huyo saleh jembe ndio mleta choko choko zote hizo kwny ishu ya morisoni yeye ndio alienda kumhoji kambini juzi kasema lamin moro hana mkataba na hachezi mechi ya mtibwa huyo saleh jembe anatumika na upande wa pili kutuvuruga tuwe makini sana na huyu m2

      Delete
  4. sasa kama mnaamini huu ni uzushi kwamba Lamine hajatamka maneno hayoo
    hebu chukueni hatua za kisheria basi ili tuamini
    maana mnapenda kudanganywa na kujidanganya mnooo
    ya Morisson yalianzaga hivi hivi mpaka leo tunasikia tuu ooooh tunaenda CAF
    shtuka na jua kutofautisha uongo na uwelii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic