UONGOZI wa simba umesema kuwa taarifa zinazoenea mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari zikieleza kuwa mchezaji wao nyota Meddie Kagere amepigana na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck sio za kweli.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa kumekuwa na taarifa ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Kagere na Sven wamepigana jambo ambalo ni la kupikwa.
"Kwetu sisi Simba ni furaha siku zote na mambo hayo yalikuwa kitambo sio sasa kila kitu kinakwenda sawa hakuna ukweli wowote kuhusu Kagere kupigana na Sven.
"Huo ni uogo na umepikwa kusudi na kwa nia ovu ya kutuvuruga kwa kuwa mambo ndani ya Simba ni shwari hivyo tumeshajua na hatupo tayari kuvurugwa.
"Ili kujua kwamba taarifa hizo ni za uongo zinaelza kwamba Kagere alipigana na kocha mazoezini, jana Simba hawajafanya mazoezi na wachezaji walilala baada ya kocha kusema kuwa wachezaji wamechoka kwa kuwa walisafiri kutoka Arusha mpaka Mbeya, hivyo kama wamepigana mazoezini ni uwanja gani walifanya mazoezi?.
"Muda huu ndio wachezaji wanajiaandaa kwenda kuanza kufanya mazoezi, hatukubali na hatupo tayari kuvurugwa," amesema.
Simba ipo Mbeya ambapo iliwasili jana Septemba Mosi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine dhidi ya Ihefu FC.
Mruhusini avae Power Bank yake.
ReplyDeleteUchawi simba , kubebwa na marefa simba, Simba ni TFF, simba wana wachezaji wazee, simba wanafanya mipango nje ya uwanja hivi ukijumlisha hivi vitu vyote hii si ni Taarabu jamani, aaaah aaah Taarabu fc tushawazoea, kauli mbiu ya mwaka huu tutawakeraaaaaaa
DeleteYanga sajili na mbembwe zote za mapokezi ya wachezaji wao wanaowaita wa viwango lakini pigo la Morrison bado linawachonota kiasi kuwa na hasira mbaya za kujitia aibu.Na hakuna zaidi wanaweza kufanya zidi ya simba isipokuwa uzushi na chokochoko zidi ya simba. Hata yale mapokezi ya wachezaji wao sio kwamba wale wachezaji ni wakali kiasi hicho kwani hakuna fowadi mpya wa yanga aliekuja mwenye uwezo wa kumzidi kagere au Kris Mugalu au Charles Ilanfiya. Na hakuna kiungo wa yanga mpya aliekuja mwenye uwezo wa kuzidi chama, Louis Miqson,Larry Bwalya,miraji Athumani,Mkude,Mudhamiri yasin,Fraga. Na hakuna Beki walioileta yanga kuzidi uwezo wa unyango au wawa na Kennedy juma.Huo ndio ukweli nuna ingia kichefuchefu chana jezi ya simba,zusha kagere mchawi au mzee na kapigana na kocha wake ila simba kwa sasa itabakia kuwa simba kwenye soka la Tanzania na east Africa na utopolo wajipike kisaikolojia kuelekea ligi kuu kwani naona wana matarajio makubwa kuliko uwezo wa timu yao watakuja kulia .
DeleteJe Sven na Kagere walipigana ama hawakupigana hii ndio hoja iliyoko mezani hizo nyingine pamoja na povu jingi havina mashiko ndugu.
DeleteKama manara anasema mambo hayo yalikuwa kitambo maana yake ilishatokea
ReplyDeleteKw hiyo kama yalishatokea we unatakaje, mpira hauchezwi kwenye mitandao ya kijamii kinachoonekana sasa hv utopolo wanatafuta Kick za kwenye mitandao ya kijamii kuliko kucheza mipra uwanjani. Tutawakeraaaaaaaa zaidi msimu huu
Deletempaka zaizi bado yanatokea isipokuwa kiukweli simba mambo yao hayavuji ovyo ila hayo mambo yapo mpaka yanasambaa mtandaoni yametoka wapi lisemwalo lipo kama halipo laja
ReplyDeleteUtopolo mmedoda uwanjani mshafeli mnatafuta ushindi nje ya uwanja hamwezi.
ReplyDeleteEnter your comment...uzush tu huo
ReplyDeleteMpeni hirizi yake mambo yarudi kama kawaida
ReplyDeleteHirizi anayo si ndo mana amekuwa mfungaji bora, sasa mnataka tumrudishie hirizi gani? na mwaka huu tumemuongezea hirizi nyingine kazi mnayo siyo 4G ni 5G, tutaendelea kuwakera wenye stress zenu huku mkijifanya mna furaha shenziiiiiiiiiiiiii. This is Simba
DeleteWamekosa cha kuongea Simba nidhamu ni kipaumbele. Walimshindwa Morisson hivyo wanadhani wote wajinga kama wao.Morisson ametulia tuli..Simba jana hawakufanya mazoezi na inadaiwa eti walipigana mazoezini jana Utopolo mpira umewashinda wamebakia na uzushi.
ReplyDeleteAnzisheni gazeti la umbeya Utopolo. Mmekuwa mabingwa wa udaku.Shigongo must be proud kupata mshindani wa udaku.
ReplyDeleteGongowazi wanaumizwa na shuari na nidhamu ya juu iliyopo kwa timu ya Manara na wanaiombea duwa Simba nayo iwe kama hali ya mvurugano na kuzomeana kama ile waliyokuwa nayo wao. Wamechelewa
ReplyDeletePiganeni tu kwani siyo Latina ukubali
ReplyDeleteWazee wameshaanza kugombana huko
ReplyDeleteUSISEME WAZEEE, SEMA WAZEE WA 4G
DeleteUnawaita wazee wakati wanakupiga 4G..bado mnawashwa mtakunwa tena nyie vijana wa chips mayai
DeleteNaye alivyozungumza kuwa kuna mchezaji mmoja amekataa kulala na mwenziwe anao ushahidi?
ReplyDeleteUmeiona picha kwenye blogu hii. UJAHILI NI UGONJWA. NA UGONJWA HUU UNAITWA UTOPOLO.
ReplyDeleteYanga ni wapuuzi sasa, wajitafakari. Mpira umewashinda imebaki kelele tuu
ReplyDeleteGongowazi ni shida. Wameunda kundi lao la waandishi na watangazaji wa michezo kwa ajili ya kuwazushia mambo mabingwa wa nchi. Unajua kila wanachofanyanya akina Maulid Kitenge, Ricardo Momo, Yusuf Mkule na wapuuzi wengine. Leo Haji Manara amewakomesha mkabaki mnajing'atang'ata tu.
ReplyDeletePiganeni sana manara atapinana na onyango
ReplyDelete