TIMU ya KMC yenye maskani yake Kinondoni itaanza msimu wa 2020/21 ikiwa na maingizo mapya 11 ndani ya kikosi cha kwanza baada ya kufanya maboresho wakati wa dirisha la usajili.
Kwenye usajili uliofunguliwa Agosti Mosi na kufungwa juzi, Agosti 31, KMC iliweza kufanya usajili wa wachezaji hao 11 ikiziba mapengo ya wachezaji wake walioondoka ikiwa ni pamoja na Ramadhan Kapera, Charlse Ilanfya.
Wachezaji hao ni Raheem Sheikh, kipa kutoka Mbao FC. Masoud Abdalah,(Dondola) kipa akitokea Coastal Union. Kenneth Masumbuko kutoka Lipuli FC.
Reliants Lusajo mshambuliaji kutoka Namungo FC, David Brayson beki wa kushoto kutoka Gwambina FC.
Beki wa kati, Lusajo Mwaikenda kutoka Azam FC,beki, Israel Patick kutoka Alliance.Kiungo mkabaji, Masoud Abdalah akitokea Klabu ya Azam FC.
Kiungo mshambuliaji, Martin Kigi kutoka Klabu ya Alliance FC. David Mwasa kutoka Lipuli yeye ni beki.
Andrew Vincent,'Dante' yeye ni beki kutoka Klabu ya Yanga
0 COMMENTS:
Post a Comment