TOTTENHAM wapo tayari kuskiliza ofa kutoka timu ambayo inamhitaji nyota wake Tanguy Ndombele ili kumuuza kiungo huyo raia wa Ufaransa.
Kiungo huyo alikuwa mchezaji muhimu wakati wa kocha Mauricio Pochettino ila alifeli kupata nafasi baada ya kocha huyo kufukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Ripoti zinaeleza kuwa kwa sasa Mourinho yupo tayari kumuuza kiungo huyo mwenye miaka 23 ikiwa tu mnunuaji atapatikana na kufikia bei ya kumnunua nyota huyo. Kocha huyo anaamini kwamba bado Ndombele hajaweza kwenda sawa na kasi ya Ligi Kuu England hivyo ana mashaka naye.
Pia sababu nyingine iliyofanya nyota huyo awekwe sokoni kwa dau la pauni milioni 54 ni kuongeza mkwanja ndani ya timu hiyo ambayo imeyumba kutokana na janga la Virusi vya Corona kuvuruga mambo kwenye masuala ya mapato.
Kwa sasa nyota huyo yupo kwenye uangalizi maalumu baada ya kukutwa na Virusi vya Corona na hayupo kwenye mpango wa Kocha Mkuu Mourinho ndani ya kikosi cha Spurs.
0 COMMENTS:
Post a Comment