September 6, 2020

 


NYOTA wawili wa kikosi cha kwanza cha Yanga leo kuna hatihati ya kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Tanzania Prisons.

Wachezaji hao ni Lamine Moro raia wa Ghana ambaye ni beki kisiki anasumbuliwa na majeraha ya goti sawa na kiungo mzawa Mapinduzi Balama ambaye anasumbuliwa pia na majeraha ya enka aliyopata msimu uliopita wakati timu ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa maendeleo ya wachezaji hao yapo vizuri hivyo kuanza kwao kikosi cha kwanza itategemea na ripoti ya daktari.

“Mpaka wakati huu maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons yapo vizuri na wachezaji wote 27 wanaendelea vema ukiachana na Balama ambaye yupo chini ya uangalizi wengine wapo fiti.

“Moro alikuwa anasumbuliwa na majeraha ila kwa sasa anaendelea vizuri ndio maana nimekwambia kwamba ukiachana na Balama wengine wote wapo fiti. Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Prisons mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Nyota hao wawili walikosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Aigle Noir uliochezwa Uwanja wa Mkapa Agosti 30 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic