BERNARD Morrison, winga mpya wa Klabu ya Simba rasmi atakipiga kwenye klabu hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kumtambulisha kwamba ni mchezaji wa timu hiyo.
Agosti 30 kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Yanga ilimtambuisha Morrison kuwa mmoja kati ya wachezaji wake 28 kwa kueleza kuwa mchezaji huyo kesi yake ipo Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Masuala ya Wachezaji,(Cas).
Mchezaji huyo pia Agosti 22 kilele cha Simba Day alitambulishwa kuwa mchezaji wa Simba na Agosti 30 jambo lililomfanya awe mchezaji pekee aliyetambulisha mara mbili ndani ya Uwanja Mkapa.
Morrison aliyekuwa na mvutano na mabosi wake hao wa zamani, alitajwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi kama mchezaji wa Yanga, akiwa jijini Arusha kukinukisha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ya timu yake mpya ya Simba iliyoishinda Namungo kwa mabao 2-0.
Lakini mashabiki wakiwa bado hawaamini kama nyota huyo aliyewapa raha msimu uiliopita kwa kuwatungua Simba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara, atasalia kikosini mwao, katika orodha ya usajili mpya ya TFF kwa msimu ujao jina lake limetokezea Simba kuonyesha ni mali yao rasmi sasa.
Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo, amesema kilichomfanya Morrison awe kwenye orodha ya Simba badala ya ile ya Yanga ni kwa kuzingatia maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliyomtambulisha kama mchezaji huru baada ya kusikiliza kesi iliyomhusisha Mghana huyo na Yanga.
Hilo limepita, ligi na ianze tuu maneno mengi ya nini?
ReplyDeleteKAMA TFF NDIO WALISUKA MIPANGO YA KUMPELEKA SIMBA ULITEGEMEA WAMUIDHINISHE AICHEZEE YANGA? DHAMBI HII ITAWATAFUNA SIMBA TFF NA MORISSON. MSIMU UJAO KUNA MTIKISIKO MKUBWA UTATOKEA KWENYE SOKA LA TANZANIA, NGUZO KUBWA ITAANGUKA.
ReplyDeleteHata malinzi akitoka jela Huwezi tena kugombea hivyo sahau kabisa kama zile za tff kuinyanyasa simba zitarudi
DeleteSawa malinzi alikuwa anawanyanyasa kwa kufungwa na kagera sugar
DeleteAcha uzembe wewe yanga na simba haya mambo wanafanyiana sana tu.ATA okwi mulivunja naye mkataba na yanga hivyohivyo na raisi alikuwa malinzi na akawatetea nyie simba mumezidi dhuruma.e
Deletetunajua mwandishi ungependa Morrison aendelee kuvaa jezi ya Yanga...acha kuendelea kuweka picha za Morrison akiwa kwenye jezi za kijana
ReplyDeleteWamesahau walivyokuwa wakishinda kwa nguvu na kupora wachezaji wa Simba chini ya TFF ya Malinzi.Sasa haki imetawala wakudeka na waliozoea kubebwa wamekuwa mabingwa wa kulalamika.
ReplyDeleteHILI SUALA LISIISHE HIVI HIVI. HAIWEZEKANI MTU AFOJI SAINI YA MCHEZAJI HALAFU ASISHTAKIWE. NATAMANI YANGA WAENDE CAS KAMA WANAVYODAI ILI WABAINIKE NA KUFUNGIWA.
ReplyDeleteYange yange Ni laana ya kukataa kumkopesha team manji, sasa inawatafuna
ReplyDeleteSasa tunae GSM ambaye ni bora kuliko Manji na
ReplyDeleteMoo anaeturejeshea furaha msimu huu na ijayo
😆😆😆😆 GSM ashawaliza kwa Morrison mkataba hewa, mnafurahisha kwelikweli. Atawakiza sana tu na kudanganywa sana tu.
DeleteTutawachania hayo mavijola yenu na kumpigeni sisi hakuna utani na nyie ohoo!
Delete