September 3, 2020


 KLABU ya Manchester United ya England imekamilisha usajili wa mchezaji Donny van de Beek (23) kwa ada ya Paundi Milioni 40 kutokea Klabu ya Ajax ya Uholanzi.

Van de Beek amesaini kandarasi ya miaka mitano kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi na inaelezwa kuwa atalipwa Paundi 107,000 kwa wiki pamoja na marupurupu.


Huu ni usajili wa kwanza wa Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa dirisha hili la usajili ambapo Van de Beek ambaye amepewa jezi namba 34 anatarajiwa kutengeneza muunganiko mzuri katika nafasi ya kiungo pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.


Solskjaer inaelezwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kusajili walau Beki mmoja wa kati na kiungo mshambuliaji wa upande wa kulia huku Jadon Sancho akiwa ndio chaguo namba moja katika eneo hilo la kiungo mshambuliaji.

2 COMMENTS:

  1. Sijui Ni kocha au uongozi wa team umelidhika man United kubaki na jina tu inabania kusajiri vijana Kama glealish na Sancho mbona wanatoa hela nyingi kwa wazee jamani sina uhakika na vanbeek anayemfahamu vzr aniambie uwezo wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni fundi hyu dogo nilimuona kwenye uefa ya msimu uliopita af ana miaka 23 tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic