Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez Septemba 7, 2020 alichaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi kuchukua nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingisa ambaye kwa sasa anafanya kazi ndani ya Klabu ya Yanga akiwa ni mshauri mkuu kuelekea kwenye masuala ya mabadiliko ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji, amesema: “Hatujakurupuka kufanya maamuzi wala sio maamuzi yangu, ni ya kikao kwani tulikaa na kuamua kumpitisha Barbara, anakuwa CEO wa kwanza mwanamke. Ni mchapakazi na anaipenda Simba, hivyo tunaamini kila kitu kitakwenda sawa.”
Akizungumza baada ya uteuzi huo, Barbara alisema: “Mimi sio muongeaji sana ila ninawaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.”
Kazi anaweza kufanya ndiyo lakini ila katika utendaji wake maamuzi yatakayo toka kwa Mo hatakuwa na nguvu ya kuyakataa kwa kuwa amewekwa na huyo.
ReplyDeleteHaija wahitokea Mo aingilie Utendaji kazi wa mtumishi wa Simba kila mmoja ana majukumu yake na anatekeleza ndiyo maana timu inasonga mbele.
DeleteHuyu ni mtendaji mkuu wa taasisi wala sio kufikiria eti atakua anafanya kwa matakwa ya Mo hiyo haihusiani kikubwa ni simba kufanikiwa kwa kiwango cha akina tp mazembe, cansablanca, mamerod n.k
DeleteBarbara ni msomi na mwenye kipaji na ujuzi Katika dunia ya soka na kutokana na mafanikio yake yanayotarajiwa, Gongowazi nao pia wataleta msichana na watafanya kama wao ndio walioanza
ReplyDeleteTuna matumaini makubwa sana na Barbara, tunaimani ataivusha Simba katika Another level.
DeleteKwa nini tunabeza kabla ya utendaji? Au ndo mfumo dume huo? Hebu tuache achape kazi na kukosoa pale atakaposhindwa. Simba siku zote inafanya selection nzuri ya watendaji wake. Haijawahi kukurupuka.
ReplyDeleteNikweli kabisa ninaunga mkono, umenena vema mungu akubariki sana.
Delete